Thursday, November 01, 2007

Jaribio la Prisons leo

Yanga leo tena inaingia katika uwanja wa Sokoine huko Mbeya kupambana na vinara wa ligi hiyo Prisons katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom.

Mpambano huo utakuwa mgumu kwa timu zote hasa ukizingatia kwamba Prisons hadi sasa imeshinda mechi zake zote ilizocheza katika uwanja wake wa nyumbani na Yanga ipo katika harakati za kutaka kujipa ahueni baada ya kufungwa na Simba wiki moja iliyopita.

Yanga inatarajiwa kuendelea kuwa na kipa mmoja tu - Jackson Chove katika kikosi chake, baada ya makipa wengine kuwa kwenye vifungo.

Kila la heri wana Jangwani, tunatarajia ushindi hii leo.

Mambo yakiwa mazuri kwenye connection ya Internet, cheki hapo chini kwenye comments ili upate kinachoendelea uwanjani ndani ya dk 90


16 comments:

Anonymous said...

Tumepata bao dk36. Mfungaji Sunguti

MOSONGA RAPHAEL said...

Mzee nimeona mambo yako kwa Michuzi kwa kuweka ukweli kuhusu kufungiwa wachezaji.
Bila shaka hapa ndipo mahali pa kupata ukweli mtupu kuhusu Yanga!
Hongera sana!!!!

Anonymous said...

Mbona kimya???Mambo yakoje????

Anonymous said...

Mrisho Ngasa anaipatia Yanga bao la pili ktk dakika ya 73.

Ni 2-0 hadi sasa

Anonymous said...

Safi sana. Naomba mambo yaendelee hivyo hivyo mpaka mwisho. Kazi nzuri CM.

Anonymous said...

Wamepata bao ktk dk85.
Ni 2-1 sasa

Anonymous said...

Mpira umekwisha kwa ushindi wa 2-1.

Shukrani kwa wote mliokuwa mnafuatilia akiwemo Bw.Mosonga.

Alamsiki!

Anonymous said...

Safi sana, hio ndo Yanga.. sio kutishiwa na vitimu kama prison...

Hongereni vijana. Mwendo huo huo.
JZah

Anonymous said...

Nasikia jana Mwaikimba na Ngassa walitisha sana! Kuna kitu kimoja kinanishangaza kuhusu Mwaikimba; akiamua kuwa serious huwa anatisha. Namuomba aendelee, hasa na hali ya sasa ambapo kuna Kabanda, Sunguti, Mwalala na Gula. Ushindani huu ufanye watu waongeze viwango. Victor ulikuwepo Sokoine hebu tupe mechi ilivyokuwa.

Anonymous said...

Naam shekhe,
Hakika jana nilikuwa mmoja kati ya wengi sana wenye furaha pale Sokoine stadium. Hakika vijana walijituma sana na ninaweza kusema pengine ndo mechi waliyocheza vizuri sana msimu huu!Defense ilijipanga vizuri sana especialy Waziri wa Ulinzi na Wisdom, kiungo nacho kilikuwa imara ingawa kutoka kwa waziri kulipunguza umuliki wetu wa hiyo idara. Kuingia kwa Mrisho Ngasa kulimaanisha kuwa beki ya Prisons ilkuwa haitakiwi kupanda sana na kwa kutolifahamu hilo ndo kulisababisha Prisons wafungwe goli la pili kwani ulikuwa ni mpira mrefu wa kutangulizwa ambao Ngasa alimzidi mbio beki na kumpiga chenga kipa kisha kuusukimizia mpira wavuni.
Kwa ujumla jana Yanga waliwamudu Prisons na hii ni mara ya kwanza katika mechi nilizoshuhudia hapa Sokoine stadium kuwaona Prisons wamebanwa. Kama kawaida, marefa na uoga wao kwa timu wenyeji waliinyima Yanga penalti 2 dhahiri ambazo laiti zingekuwa the other way angewapa Prisons penalti kama walivyofanya ktk mechi ya Prisons na Manyema.
Chove,Mbuna,Mtiro,Wisdom,Hamisi,Abuu,Mwaikimba,Sunguti jana walifanya kazi nzuri sana pia Mrisho na Canavaro walileta mabadiliko mazuri.
Ni ukweli jana Mwaikimba was the best player on the pitch na sina hakika tatizo huwa ni nini maana hakuwa yule Mwaikimba niliyezoea kumuona kwenye uwanja wa taifa dar. Alimiliki vema mipira na kuwalisha wenzake mipira ya uhakika na hata ile mipira ya vichwa alikuwa anawadondoshea vizuri sana wenzake. Kingine kikubwa kwa Mwaikimba jana ilikuwa ni jinsi alivyoweza kuwakeep ocupied mabeki wote wa Prisons. Kama Gaudens ataendelea hivi nina hakika atarudia makali yake aliyokuwa nayo.
Mwisho nampa big up kocha Chamangwana,alipofika hapa Mbeya waandishi wa habari wote maswali yao yalikuwa juu ya wachezaji nyota ambao hawakuja huku Mbeya ila yeye jibu lake lilikuwa ni moja tu,"Hawa waliopo ndio wachezaji wa Yanga!". Amewaamini wapiganaji waliopo so hata sisi washabiki tuwaamini,yeyote aliyesajiliwa Yanga anapaswa kupewa nafasi aonyeshe uwezo na mifano mizuri ni Chove,Mbuna na Abuu Ramadhani .
I hope kwa kiasi fulani Chris utakuwa umepata picha what went on hapa Mbeya, i hope going forward mambo yatakuwa mazuri zaidi kwa Yanga!!
Mungu ibariki Yanga.

Anonymous said...

Hawa vijana wetu wanaanza kucheza mpira wa maana wakati ligi inaelekea kwenye mapumziko.

Muda huu wa mapumziko kwa vile safari hii hatuna wachezaji wengi katika timu ya Taifa, basi ni vizuri hawa vijana wakaendelea na mazoezi na mechi za kujipima nguvu ili tumalize ngwe ya pili katika form tuliyo nayo sasa.

Anonymous said...

Naungana na mdau hapo juu kupendekeza timu iwekwe kambini tena nje ya mji kwa mazoezi zaidi, baada ya hii round ya kwanza. Kama uongozi unaweza kuomba kule bulyanhulu, nasikia kuna uwanja mzuri tuu na facilities zingine za training. Tena huu ndo wakati mzuri wa makocha wapya kuanza kazi (kama kweli wanasaini mkataba), sio kusubiri round ya pili imeanza na makocha wapya ndo wanapewa timu halafu tunaanza kulaumiana.!

Napendekeza yafuatayo kuhusu timu na makocha wapya:

1. Chamangwana aendelee kusaidiana na makocha wa kigeni kuinoa timu. Benchi la ufundi liwe na makocha wanne, Chamangwana, Siwa, na hao Wa-serbia wawili. Kuwe na program ya muda mrefu na mfupi. Timu iwe na wachezaji zaidi wale wanaocheza ligi. Yaani, kuwe na kama wachezaji 11 vijana (under 20) ambao wana-train na timu ya wakubwa wakitafuta namba, kama ilivyo kwa Jerry Tegete sasa hivi. Ikitokea nafasi, basi anapandishwa mchezaji toka kwenye hili group. Wachezaji hawa watasaidia timu kuzoeana kiuchezaji, kuliko sasa ambapo kila msimu timu inakuwa mpya 10.

2. Chamangwana apewe msaidizi kuendeleza timu za vijana (under 18 na under 16). Huyu kocha msaidizi, napendekeza awe mmoja wa wachezaji wa zamani. Program ya timu za vijana iwe synchronised na timu za wakubwa, yaani vijana wakue-toka u16 to u18 na baadaye u20 ambao wata-train na timu ya wakubwa.

Kwa hiyo Jack atakuwa kama link ya timu za vijana na wakubwa.

Tukifuata mfumo kama huu ambao pia unatumiwa na timu kubwa za ulaya, hatutahitaji kusajili wachezaji wapya kila mwaka. Na wale watakaopandishwa hawatakuwa wageni.

Mfumo huu pia ndio utakaowezesha Yanga kuuza wachezaji Ulaya. Ni vigumu sana kwa kina Nsajigwa na Mwaikimba kuchezea Chelsea na timu zingine, sababu wanaanza kuonekana wakati tayari wako over 25!

Wadau wengine mnaweza kuchangia mawazo yenu, na viongozi wanaweza kupata mawazo mazuri hapa ...!

JZah,

Anonymous said...

Habari wote,
Mawazo yaliyotolewa na wadau hao hapo juu ni sahihi kabisa na ni njia nzuri sana ya kupata maendeleo ya uhakika kwa Yanga. Kwa wakati huu ambao tunaye mtu ambaye tuko willing ku-bankroll maendeleo yetu ni muda muafaka kwa viongozi kuibuka na mawazo kama hayo hapo juu!Chamangwana wakati yuko hapa Mbeya alilalamika wazi kuwa sasa timu inaanza kupata mwenendo mzuri ndio hii long break inakuja, hata yeye yuko of the opinion kuwa timu iendele na mazoezi.
Kuwa na timu ya vijana itatusaidia sana kutohangaika wakati wa usajili ila pia kwenye huu usajili makocha waachwe wafanye kazi yao na sio viongozi kusajili ili kufurahisha tu wanachama huku wachezaji wapya wakiwa na msaada mdogo sana kwenye timu.
Shime washabiki, endeleeni kutoa michango ya kusaidia timu kama ya hao jamaa wawili hapo juu!!
All the best!!!!!

Anonymous said...

[B]NZBsRus.com[/B]
Forget Sluggish Downloads With NZB Downloads You Can Rapidly Find High Quality Movies, Console Games, MP3s, Applications & Download Them at Rapid Speeds

[URL=http://www.nzbsrus.com][B]Usenet Search[/B][/URL]

Anonymous said...

Predilection casinos? weed somewhere else this advanced [url=http://www.realcazinoz.com]casino[/url] superintend and toady to online casino games like slots, blackjack, roulette, baccarat and more at www.realcazinoz.com .
you can also delay our hip [url=http://freecasinogames2010.webs.com]casino[/url] trade something at http://freecasinogames2010.webs.com and turn back in chief folding deviation !
another contributory [url=http://www.ttittancasino.com]casino spiele[/url] core is www.ttittancasino.com , during german gamblers, submit c be communicated sooner than unrestrained online casino bonus.

Anonymous said...

I think this is among the most significant info for me.
And i'm glad reading your article. But should remark on few general things, The web site style is ideal, the articles is really excellent : D. Good job, cheers

Review my website :: netent casino no deposit