Monday, November 19, 2007

Yanga kulikoni?

Ningependa kuomba radhi wapenzi wadau wa blogu yetu hii kutokana na kutokuwa na post mpya kwa siku kadhaa hii inatokana na hali ya ukimya uliotanda ndani ya klabu yetu.

Mengi yaliyokuwa yanazungumzwa yalikuwa hayathibitishwi kwa vile viongozi wakuu walikuwa kwenye semina elekezi iliyoandaliwa na FIFA huko Bagamoyo.

Dondoo za yale yaliyokuwa yakizungumzwa:

  • Wachezaji kadhaa bado hawajaweka sahihi zao katika fomu za usajili wa klabu hiyo kwa ajili ya michuano ya CAF kwa sababu mbalimbali lakini kubwa ni la kumalizika kwa mikataba yao. Miongoni mwa wachezaji hao ni Thomas Mourice, Edwin Mukenya na Amri Kiemba. Pia wachezaji wengine kama Ivo Mapunda na Shadrack Nsajigwa inasemekana wamenyimwa fomu za usajili. Hali hii ya sintofahamu imeifanya klabu hii kushindwa kuwasilisha fomu zake katika Shirikisho la soka nchini TFF hadi hivi sasa.
  • Suala la makocha wapya kutoingia mkataba hadi hivi sasa bado linawachanganya wadau wa Yanga kwani ni muda mrefu sasa umepita tangu wataalamu hao watue nchini. Miongoni mwa sababu zinazotolewa ni ...Manji hayupo nchini au viongozi wapo nje ya Dar
Ni hayo tu kwa sasa.

1 comment:

Anonymous said...

Kuna habari kuwa makocha wame-sign mikataba (sijui ya mwaka au miaka miwili).

Kina Ivo na Nsajigwa, napendekeza wasainishwe form za CAF na wapunguziwe adhabu zao. Iwe ni miezi miwili au wasamehewe kabisa. Round ijayo tuanze bila migogoro na fitina.

JZah