Monday, December 24, 2007

Heri ya Krismasi



Ningependa kuwatakia wadau wote wa blogu hii heri ya sikukuu ya Krismasi.

Ni kipindi kizuri ambacho watu tunajumuika pamoja na ndugu, jamaa na marafiki katika kusherehekea sikukuu hii.

Kwa vile tumekuwa pamoja mara kwa mara katika blogu hii, nawachukulia ninyi kama jamaa zangu wa karibu hivyo basi si vibaya mkazipokea salamu hizi za heri.

Nawashukuru wale wote waliotumia muda wao katika mwaka huu kupita katika blogu hii - iwe ni kwa kutuma maoni na hata kwa kusoma tu post. Ningependa maoni zaidi kwani hii itasaidia kuboresha blogu yetu. Kwa siku chache zilizobaki kabla ya kufunga mwaka naomba kusikia maoni yenu na ikiwezekana kama unaona maoni yako ni marefu sana basi nitumie email kupitia (yangatz@yahoo.com). Ni vizuri ukiniambia uko wapi ili nijue blogu hii ina wadau kutoka katika nchi gani.

Hata wale ambao huwa hawachangiii mnaweza tu kuwatakia wadau wenzako heri ya sikukuu. - Utani tu

Mungu awazidishie heri na baraka.


4 comments:

Anonymous said...

Napenda kuwatakia wadau wote wa blog hii heri ya Krismas na mwaka mpya. Pili kumshukuru mwanzilishi wa kilinge hichi, maana ni mahali pekee tunapata habari motomoto kuhusu klabu kipenzi chetu.

Ingawa wadau wengi hapa watakuwa pia wapenzi wa timu zingine za ulaya, lakini mapenzi kwa timu kama Yanga yanakuwa ya dhati, na ikifanya timu vibaya inakuuma kweli!

Kuhsu namna ya kuendeleza blog hii (na klabu yetu kwa ujumla) napendekeza yafuatayo:

1. Katika mwaka ujao, inaonekana so far timu inaandaliwa vizuri. Kama itawezekana kuwe na live (online) coverage ya kila mechi (hasa za kimataifa zitakazochezwa Dar).

2. Tuweke mkakati wa kutunza statistics za wachezaji wetu. Like, mchezaji amecheza mechi ngapi, dakika ngapi, amefunga magoli mangapi, kadi ngapi n.k. Then mwisho wa mwezi tuweke summary ya performance ya kila mchezaji.

3. Tuangalie namna ya kuisaidia klabu yetu kuongeza mapato yake kupitia souvenirs and momentos, au njia nyingine. Watani zetu walianzasha lottery, ambayo ingawa nasikia imewaingizia hasara, I still believe it was a good idea. Tunaweza ku-brainstorm hapa na kupata mawazo mengi mazuri ya kuisaidia klabu ijitegemee, somehow.

4. Napendekeza pia tuwe tunapata maendeleo ya timu ya vijana, kama kuna wachezaji wangapi, wanafanya nini, schedule yake n.k. Pia nina swali: Je Siwa naye yuko na Chamangwana kwenye hii timu au ameondoka? Yeyote mwenye details..!

4. Napendeza kupitia matawi yetu, vianzishwe vikundi vya ushangiliaji hasa kwa mechi za kimataifa, ambavyo vitawapa wachezaji hamasa muda wote wa mchezo kwa kushangilia.

Ni hayo tuu kwa sasa, wengine pia mwakaribishwa.

JZah,
Washington DC, USA.

Anonymous said...

Tuanzishe umoja wa washabiki wa Yanga ambao utatambuliwa na uongozi wa Timu.
Pia tunaweza kuwa tunaushauri uongozi ktk masuala mbalimbali na pia kutetea maslahi ya washabiki wa Yanga.
Tuwe na katiba yetu na ada ya uanachama. Ila ni muhimu tuwe na maelewano hai na uongozi halali wa timu.
Tunaweza pia kutumia umoja wetu huo kuomba mgao wa tiketi za kushuhudia mechi na umoja unawalipa Yanga moja kwa moja.
Hongera Yanga kwa maendeleo mazuri huko South Africa.

Heri ya mwaka mpya 2008.

Mdau kutoka Berks, England.

Anonymous said...

Naongezea kuwa kuhusu mgao wa kadi ni kwamba Umoja wa mashabiki wa Yanga utakusanya hela za wanaotaka kuingia mechi za Yanga halafu unaomba idadi halisi ya tiketi ktk mechi husika.
Kwa hiyo umoja unakuwa kama agency!
Hii itapunguza usumbufu wa kila mtu kuweka foleni kununua tiketi.

Anonymous said...

Yanga Fans Club (YFC) together with Yanga SC