Wednesday, December 05, 2007

Kombe la Shirikisho Afrika:
Yanga yavuka hadi Raundi ya kwanza



Shirikisho la soka Afrika CAF jana lilitoa ratiba ya michuano yake kwa upande wa vilabu ambapo Yanga imeingizwa moja kwa moja katika hatua ya raundi ya kwanza kufuatia soka la Tanzania kupanda katika miaka ya hivi karibuni.

Yanga imepangiwa kucheza na mshindi wa mchezo wa raundi ya awali ya michuano hiyo kati ya AL AKHDAR ya Libya na Mwakilishi kutoka nchi ya Chad.

Katika mchezo huo wa raundi ya kwanza utakaofanyika kati ya tarehe 21,22 au 23 ya mwezi wa Machi mwakani, Yanga itaanzia nyumbani.

Haya sasa Waarabu wengine haoooo wanakuja.

No comments: