Tuesday, December 18, 2007

Kombe la Shirikisho Afrika:
Yanga yarudishwa raundi ya awali
Shirikisho la soka Afrika CAF limefanya mabadiliko ya ratiba ya michuano ya Kombe la Shirikisho ambapo sasa Yanga itaanzia raundi ya awali kwa kupambana na AS Adema ya Madagascar.

Katika raundi hiyo, Yanga itaanzia ugenini huko Antananarivo kwenye Uwanja wa nyumbani wa AS Adema unaojulikana kama Mahamasina. Mchezo huo utapigwa kati ya tarehe 15/16/17 Februari 2008 na marudiano itakuwa hapa Dar kati ya tarehe 1/2 Machi 2008


Yanga ikifanikiwa kuvuka raudi hiyo, itakumbana na mshindi kati ya
Al Akhdar(Libya) na mwakilishi kutoka Chad katika raundi ya kutafuta 16 bora.

Baada ya hapo kama tena Yanga itavuka raundi hiyo, itaingia kwenye hatua ya kutafuta nane bora ambapo itakumbana na mshindi kati ya Haras El Hodoud(Misri) na MC Alger(Algeria).

Safari ni ndefu kwa kweli. Naona njia yetu imejaa nchi za Kiarabu na historia yetu na vilabu vya nchi hizo si ya kuridhisha. Hata hivyo penye nia pana njia.


1 comment:

Anonymous said...

Dhidi ya klabu za Madagaska, Libya/Chad tunaweza kuvuka - hakuna wasiwasi (lakini juhudi ni muhimu, tusilale!).

Kwa upande wa timu za Misri/Algeria itabidi Yanga waongeze bidii na maarifa - sio mechi rahisi hizi.

Timu ya vijana Yanga ni muhimu kwa kuinua vipaji vya chipukizi.