Friday, December 21, 2007

Kundi la pili kuondoka kesho

Wachezaji 5 wa Yanga waliokuwa wakichezea timu za Taifa za Tanzania Bara (Kilimnjaro Stars) na Tz Visiwani (Zanzibar Heroes) wanatarajiwa kuondoka kesho kwa ajili ya kuungana na wenzao ambao wapo huko Afrika ya Kusini kwa ajili ya kambi ya mazoezi.

Wachezaji hao Amir Maftah, Castory Mumbala na Vincent Barnabas waliokuwa K'njaro Stars pamoja na Abdi Kassim na Nadir Haroub waliokuwa Z'bar Heroes wamepata nafasi hiyo baada ya timu zao kuondolewa mapema katika michuano ya kombe la Challenge inayoendelea Jijini Dar es Salaam.

Hata hivyo bado wachezaji Ivo Mapunda na Shadrack Nsajigwa watabaki nchini kuendelea kutumikia adhabu zao za kutocheza soka kwa miezi sita.

Mshambuliaji Ben Mwalala licha ya kurejea, anatarajiwa kubakizwa nchini hadi hapo uongozi utakapokaa na kusikiliza utetezi wake ni kwanini amechelewa kuripoti kambini kwa muda wa wiki mbili.


2 comments:

Anonymous said...

Ndugu nafurahi sana kusikia kuwa Yanga imewafikiria pia wachezaji watano ambao walikuwa Zanzibara heroes na Kilimanjaro stars. Ni jambo jema. Nimefurahi pia kusikia kuwa Mwalala hataenda huko Bondeni. Huyo Mwalala anatupotezea muda wetu mimi naona hata angepigwa buti asichezee yanga kabisa maana anaharibu hata mori ya wenzake.

JAMBO JINGINE MIMI NAOMBA HAWA VIONGOZI WETU WAWASAMEHE IVO NA NSAJIGWA KWA MASHARTI. NI MUHIMU PIA KUPATA HUTUMA YAO MAANA NI WACHEZAJI WAZURI. WACHEZAJI WAAMBIWE WASIRUDIE TENA MAKOSA YAO NA WAKIRUDIA WAFUKUZWE KABISA (AMEONDOKA HENRY WA ASERNAL ITAKUWA WAO?)

Anonymous said...

Yanga ni timu nzuri na tungependa wachezaji na viongozi wetu washirikiane sana. Tatizo moja ninaloliona ni kuwa viongozi wetu wa mpira wanakuwa na tamaa sana ya kusajiri wachezaji wapya. Kila mwaka Yanga inasajili wapya hivyo inakuchukua muda sana kwa wachezaji kuelewana. Tujaribu kudumu na timu na kama ni usajiri uwe wa wachezaji wachache sana.

aak