Monday, January 28, 2008

Yanga bado?

Ushindi wa 2-1 wa Yanga hapo Jumamosi dhidi ya Ashanti United umepokelewa kwa hisia tofauti na mashabiki wa klabu ya Yanga.

Wapo wanaosema kwamba pamoja na ushindi huo lakini timu ilicheza mchezo mbovu na pia wapo wanaosema kwamba ni kawaida kwa mechi inayokutanisha timu zinazotoka sehemu moja (local derby games) huwa kuna hali ya kukamiana sana kiasi kwamba ufundi wa mpira unakuwa mdogo sana.

Kwa wenye mawazo ya pili naweza kukubaliana nao kwani mechi ya Jumamosi, wachezaji wawili wa Yanga - Hamisi Yusuf na Athuman Iddi walicheza na bandeji kichwani kutokana na misukosuko ya mechi hiyo ilihali wachezaji Hussein Kaongo wa Ashanti na Credo Mwaipopo wa Yanga nao walikimbizwa hospitali kutokana na mikikimikiki ya mechi hiyo.

Nafikiri tuendelee kuangalia mechi nyingine kama mbili hivi tuone hali halisi ya timu yetu. Kwa wale wadau wezangu mliokuwepo uwanjani mnasemaje?

5 comments:

Anonymous said...

Ni kweli, bora tuwape muda tuwaone vizuri.

Anonymous said...

Kondic ananitia wasiwasi sana na uwezo wake.Anakemea wachezaji wazi wazi.Baada ya mechi na Ashanti alikuwa akipiga kelele na kuwaponda washambuliaji akimweleza Fred Mbuna huku wengine wasiohusika wakisikia.Morale ya wachezaji inaathirika kutokana na kocha huyu kkukosa ethics na utaalamu wa kuweka mambo sawa.Kama ana la kusema angengoja muda muafaka sio kutoa vitisho kwamba nataka wachezaji wote kesho saa kumi na mbili asubuhi na kadhalika.Tumeshinda ni hivyo je tukifungwa????

Anonymous said...

Huyo kocha wetu Kondic amekuwa kama konda! anapenda kuchonga sana. Tuwaomba viongozi wetu wajaribu kuongea naye. Siyo kwa kuwa mshahara wake unatoka kwa Manji ndiyo alete za kuleta. Aache kuchonga hii ni Dar bwana akituletea tutamfyatua aeende kwao. Nawatakia ushabiki mwema.

Baba Kelvin wa Temboni.

Anonymous said...

Wadau wawili hapo juu mmeniacha hoi kwa kicheko. Mimi nadhani kocha ni binadamu na ana style yake ya ufundishaji na ku-react to situations. Huwezi kumfananisha Morrino na Wenger!

Ni kweli kwamba hakufurahishwa na ushindi uliopatikana, na pale uwanjani ndio ofisini kwake, sasa kwa nini asubiri kuonesha emotions zake kwa siri.

Wachezaji wamwelewe mwalimu na wafuate anachotaka, yeye ndio manager wao. Ni wakati wa Uwazi na ukweli! Sidhani kama mwalimu angegogomba iwapo hizo nafasi zilizopatikana zingetumiwa kupata mabao. Na hicho ndio kinatakiwa.

Washambuliaji wawe na uchu wa kufunga kila nafasi inapopatikana. Tuliwahi kuwa na wachezaji wa aina anayotaka mwalimu, kwa hiyo sio kwamba anaongea kitu kigeni.

Anonymous said...

Mwalala na Maftah wamesamehewa!!Nilisema kabla uongozi hauna ubavu wa kumwadhibu Mwalala.Na kuhusu Maftah mbona kosa lake sawa na kina Ivo au nakosea kwanini yeye asamehewe??Kuna tabaka ndani ya timu yetu??Au wapo wanaolindwa???