Tegete, "Cannavaro" waibeba Stars
Mabao mawili yaliyofungwa na wachezaji Jerry Tegete na Nadir Haroub "Cannavaro" leo jioni yalitosha kuivusha Taifa Stars katika hatua ya pili ya michuano ya Ubingwa wa Afrika (kwa wachezaji wa ndani) - baada ya kuifunga Harambee Stars ya Kenya 2-0 katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Katika mchezo wa awali uliopigwa huko Nairobi, Taifa Stars ililala 1-0, hivyo basi Taifa Stars inasonga mbele kwa 2-1 ambapo sasa itakutana na Uganda Cranes iliyoitoa Eritrea kwa jumla ya 5-2. (3-0, 2-2).
Tunawapongeza vijana wetu wa kwa kuweza kuipaisha Stars kama mnavyoipaisha Yanga.
4 comments:
Vipi mpira leo?
jamaa naomba frequence ya gtv nasi tuone mpira wa yanga na prison pia yanga na simba mdau m sakran kuwait
GTV ni kituo cha kulipia, hivyo kwa wale tu walio na subscription ndiyo watakaofaidi uhondo.
Kwa wale tulio USA, ni channel ipi inarushwa hawa GTZ?
Post a Comment