Thursday, April 03, 2008

Wadau mnasemaje?

Yanga inatarajiwa kuingia uwanjani keshokutwa kupambana na Al Akhdar ya Libya katika mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho barani Afrika.

Al Akhdar inatarajiwa kuwasili hapo kesho mchana huku ikiwa na kazi ya kulazimika kutikisa nyavu za Yanga angalau mara mbili huku Yanga ikiwa na kumbukumbu ya sare ya 1-1 iliyoipata wiki mbili zilizopita huko Tripoli.

Wadau vipi mnazungumziaje hii mechi?

4 comments:

Anonymous said...

nawaombea kila la kheri kwa jinsi nilivyoona mechi ya kwanza ugenini vijana walitawala sehemu kubwa ya mchezo nategemea tatu bila kila la la kheri m sakran kuwait

Anonymous said...

Ninawatakia kila la kheri wachezaji wote. Nawaomba pia wapenzi wote wajitokeze kwa wingi na kuwapa moyo wachezaji kwa kuwashangilia mwanzo hadi mwisho. Ni kweli ushindi unawezekana, ila pia tunatakiwa kucheza kwa tahadhali kubwa maana wao hawana cha kupoteza zaidi,.. kwa hiyo watakuwa wanashambulia tuu ili angalau wapate bao la mapema.

Zack,

Anonymous said...

Yanga wanatakiwa kuelewa kuwa kazi bado haijaisha.

Kama kawaida watumie karibu kila nafasi wanayopata.

Wajifunze kupiga set-pieces (free kicks, kona) ili ziweze kuzaa matunda. Mara nyingi ktk mpira wa miguu nafasi huwa haba za kufunga hivyo ni vema kutumia vizuri mipira ya adhabu.

Kitu kingine cha muhimu ni upigaji wa mikwaju ya penalti. Ni vizuri robo tatu ya wachezaji wote wawe na uwezo wa kupiga penalti. ikipatina moja itumiwe vema. Lakini matokeo yakiwa tena 1-1 basi Yanga wawe tayari kuwa na wapigaji wa uhakika angalau 7.

Anonymous said...

nawatakia kila la kheri timu yangu ya yanga ila tatizo yanga hii iliyo na maisha bora ile mby katika timu za east africa ka pesa haioneshi mpira unaotegemewa,mpira upo chini ile mby niliwaona mwz walipocheza na toto ni bomu japo walishinda hivi ni kwanini?soka iwe na radha jamani sio kuongoza tu ligi ila soka kiny'aa