Saturday, May 24, 2008

TAIFA STARS special

Maximo kujaribu kikosi na Malawi

Timu ya soka ya Taifa ya Tanzania kesho inajitupa katika Uwanja mkuu wa Taifa wakati itakapopambana na timu ya Taifa ya Malawi (The Flames) katika mchezo wa kirafiki wa kujipima nguvu.

Taifa Stars wiki ijayo inakabiliwa na kipute cha ufunguzi wa kampeni yake ya kucheza fainali za Kombe la Afrika huko Angola pamoja na Kombe la Dunia huko Afrika ya Kusini 2010 kwa kupambana na Mauritus.

Katika mchezo wa kesho, Stars sasa itaweza kuwatumia wachezaji wake wanaosakata kabumbu nje baada ya kukosa michezo 4 iliyopita kufuatia kubanwa na sheria iliyokuwa inaongoza michuano ya wachezaji wanaocheza ligi za ndani ya nchi (CHAN).

Kila la heri Taifa Stars

3 comments:

Anonymous said...

vipi matokeo bado?

Anonymous said...

vipi tumelala?

Anonymous said...

Tumetoka sare ya 1-1.
Stars ilitangulia kufungwa lakini ilifanikiwa kusawazisha kupitia kwa beki Salum Sued