Saturday, June 28, 2008

Kagame Cup: Tupo kundi "C"

Mabingwa wa soka nchini Yanga wamepangwa katika kundi "C" la michuano ya Kombe la Kagame litakaoanza kutimua vumbi kuanzia Julai 12 Jijini Dar es Salaam.

Yanga inayoingia katika michuano hiyo kama mshindi wa pili wa ligi ndogo ya TFF 2006/07, imepangwa kundi moja na mabingwa watetezi ARP ya Rwanda, Awassa City ya Ethiopia pamoja na Miembeni ya Zanzibar.

Jumla ya timu 11 zinatarajiwa kushiriki michuano hiyo ambayo mshindi huweka kibindoni dola za Kimarekani 30,000, mshindi wa pili dola 20,000 na mshindi wa tatu dola 10,000.

Makundi mengine katika michuano hiyo ni Kundi A: URA (Uganda) , Rayon Sports (Rwanda), Den Den(Djibouti) na SID(Somalia). Kundi B lina timu za Simba(Tanzania), Vital'O (Burundi), Tusker (Kenya) na Benadir (Somalia).

Wakati huo huo michuano ya CECAFA (ya mataifa) kwa mwaka huu yatafanyika Jijini Kampala nchini Uganda kuanzia Novemba 8 hadi 23 mwaka huu.


No comments: