Monday, June 09, 2008

Kaseja?
Juma Kaseja Juma

Magazeti kadhaa yameripoti leo juu ya kusajiliwa kwa Kipa wa zamani wa Taifa Stars Juma Kaseja katika kikosi cha Yanga kwa ajili ya msimu ujao.

Hadi sasa hakuna taarifa kamili iliyothibitishwa kuhusu hilo lakini ninafanyia kazi taarifa hizo.

Endapo taarifa hizo zitakuwa ni za kweli basi watu watajiuliza ni kwa vipi Yanga imsajili Kaseja wakati kuondoka kwa kiungo wa timu hiyo Athuman Iddy katika timu ya Simba kwa kiasi kikubwa kulisababishwa na Kaseja?

Mojawapo ya habari za usjili huo cheki hapa

4 comments:

Anonymous said...

habari ni za kweli, nimezithibitisha mwenyewe toka kwa kocha wa simba Julio wakati tukiwa katika kambi ya vijana wa copa coca cola pale mabibo hostel

Anonymous said...

1. Sina tatizo na Kaseja kusajiliwa Yanga, lakini sababu zake kuwa amefuata tuu maslahi hairidhishi.

http://mwananchi.co.tz/newsre.asp?id=6100

Ni kweli soka ni ajira na sii mapenzi, lakini maslahi haipaswi kuwa sababu pekee ya kumleta Yanga.
Ina maana maslahi yakiisha ataondoka siku hiyo hiyo atarudi Simba?

2. Kama kuna tatizo kati yake na Athumani Iddi, naamini linaweza kumalizwa kwa mazungumzo. Kwani Kaseja akiitwa timu ya taifa, Iddi atajitoa?

3. Viongozi wawe makini na hawa wachezaji wa Simba. Naamini wanaitumia Yanga kuboresha maslahi yao huko Simba. Viongozi wasipoangalia mwishoni timu itakuwa haina kipa na wachezaji wengine muhimu, maana 'Friends of Simba' wakifika dau hata leo Kaseja ataondoka zake tuu (anachoangalia ni maslahi .. maneno yake mwenyewe).

Tuwape nafani wachezaji chipukizi toka kikosi cha Chamangwana badala ya kutumia hela kibao kusajili mchezaji atayakeyakaa kwa msimu mmoja! Hizo hela zitumike kuwakweka kabini na kununua vifaa vya mazoezi.

Zach.

Anonymous said...

Mpira na kazi, hata huku Ulaya wachezaji haana timu anakwenda anapohitajika, hizo fikira za kuwa mchezaji lazima awe mpenzi wa timu zimepitwa na wakati

Anonymous said...

nakuunga mkono mzee,mchezaji hachezei mapenzi tu klabu siku hizi.Hiyo ni ajira kama ajira nyingine.Hivyo,usitegemee mchezaji awe na malipo hafifu halafu aendelee kukaa kwenye klabu kwa mapenzi.Mpira huo umepitwa na wakati.