Tuesday, August 12, 2008

10 wa Yanga waitwa Stars

Mabingwa wa soka nchini Yanga imetoa jumla ya wachezaji 10 kuunda timu ya Taifa ya soka ya Tanzania - Taifa Stars iliyotangazwa jana na kocha wa timu hiyo Marcio Maximo.

Katika orodha hiyo, Juma Kaseja ameendelea kuachwa katika kikosi hicho huku kipa wa Simba, Amani Simba amebahatika kuitwa katika kikosi hicho kwa mara ya kwanza.

Kikosi kamili amabcho alikitangaza Maximo kwa ajili ya michuano hiyo ni makipa; Ivo Mapunda (Yanga), Farouk Ramadhani (Miembeni) na Amani Simba (Simba).

Mabeki ni Shadrack Nsajigwa, Amir Maftah, Fred Mbuna, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ (Yanga), Juma Jabu, Kelvin 'Vidic' Yondani, Meshack Abel, (Simba) na Salum Sued wa Mtibwa Sugar.

Aliwataja viungo kuwa ni Athuman Idd, Kiggi Makasi na Godfrey Bonny (Yanga), Henry Joseph, Jabir Aziz, Adam Kingwande (Simba), Shaaban Nditi (Mtibwa) na Nizar Khalfan (Moro United).

Kwa upande wa safu yake ya washambuliaji waliochaguliwa ni Mussa Hassan Mgosi (Simba), Uhuru Selemani (Mtibwa), Jerry Tegete na Mrisho Ngassa (Yanga).

Kwa upande wa vijana ambao Maximo amesema kazi yao itakuwa ni kujifunza, ni Jonas Salvatory na Yusuf Soka (chini ya miaka 17 mwaka 2007), Adili Adam na Lambere Jerome (chini ya miaka 17 mwaka 2008) na Awasi Issa kutoka chini ya miaka 20.

- Kibwagizo: Eti ni kweli Nurdin Bakari na Ramadhan Chombo 'Redondo' wamesahaulika?

No comments: