Blogu binafsi kwa ajili ya wapenzi na wanachama wa Yanga popote pale ulimwenguni kubadilishana mawazo na kupashana habari
Wednesday, August 13, 2008
TFF bado yajiuliza
Katika hali inayoonyesha kutokubaliana na maamuzi ya Kamati ya Nidhamu ya TFF, Shirikisho la soka nchini TFF bado haijaridhia uamuzi wa kufutwa kwa adhabu iliyokuwa ikiikabili klabu ya Yanga.
TFF wanaweza kabisa kukataa kutambua maamuzi ya kamati ya nidhamu.Rage alikata rufaa kwa kamati hiyo na kamati ya utendaji ikakataa kutimiza hukumu ya kamati hiyo na alipoongea na FIFA wakamwambia angojee uchaguzi wakiwa wanakubaliana na kamati ya utendaji.Kamati ya utendaji ni chombo cha juu kikatiba kwenye TFF na maamuzi yao yanaweza kutenguliwa na mkutano mkuu tu.Ninachoogopa TFF wakiiarifu CAF basi uwezekano wetu wa kushinda ni mdogo sana hivyo busara zitumike na tuache malumbano.
El Maamry tayari ametoa ushauri kwamba kamati ya Utendaji iachane na mambo ya kutoa adhabu badala yake ibakie na masuala ya sera tu.
Hii kwa kiasi kikubwa italeta maana halisi ya kamati ya Nidhamu.
Hapa tayari El Maamry ameshaweka wazi kwamba hakuna kanuni ya kuifungia timu kwa miaka 2 kucheza michezo ya kimataifa kwa kosa la kutokwenda uwanjani lakini kamati ya utendaji ya TFF inataka kuonyesha ubavu wake, sijui tutaishia wapi.
6 comments:

TFF hawana upeo wa kutosha! Wanafanya mambo au maamuzi kienyeji sana!!
TFF inahitaji kufanyiwa 'M.O.T' ya hali ya juu, ili soka nchini iende mbele kwa mazingira ya leo ktk dunia ya mpira!
Mdau, UK
El Maamry tayari ametoa ushauri kwamba kamati ya Utendaji iachane na mambo ya kutoa adhabu badala yake ibakie na masuala ya sera tu.
Hii kwa kiasi kikubwa italeta maana halisi ya kamati ya Nidhamu.
Hapa tayari El Maamry ameshaweka wazi kwamba hakuna kanuni ya kuifungia timu kwa miaka 2 kucheza michezo ya kimataifa kwa kosa la kutokwenda uwanjani lakini kamati ya utendaji ya TFF inataka kuonyesha ubavu wake, sijui tutaishia wapi.
tunataka kuona hiyo kanuni kwa maandishi, kama kweli yanga inasthili hiyo adhabu, la sivyo hao tff ni maninja tu.
Mikojo imeanza kuwatoka na mbado.
WE PANYA UMEPENYEZAJE?
Post a Comment