Tuesday, September 16, 2008

TFF kuijadili Yanga Septemba 27
Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la soka nchini (TFF), itakutana Septemba 27 mwaka huu kujadili mambo mbalimbali ikiwemo kutenguliwa kwa adhabu ya Yanga.

Akizungumza na waandishi wa habari hapo jana, Katibu Mkuu wa TFF Frederick Mwakalebela amesema kwamba kamati hiyo itakutana ikiwa na agenda tatu mojawapo ikiwa ni kupitia uamuzi wa Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho hilo kuifuta adhabu ya kuifungia Yanga kwa miaka miwili kucheza michezo ya kimataifa nadai na nje ya nchi.

Adhabu hiyo ilipunguzwa na kamati ya nidhamu chini ya Said El Maamry na kuamua kuitoza Yanga dola za Kimarekani 20,000 ambazo tayari zimepokelewa na TFF huku wakisubiri uamuzi wa mwisho wa Kamati ya Utendaji hapo Septemba 27.

No comments: