Saturday, September 13, 2008

Yanga kibaruani kwa Mtibwa

Wakati kukiwa na mvutano kuhusu mkutano mkuu wa wanachama, timu ya Yanga leo inajitupa kwenye Uwanja wa Jamhuri Morogoro kwa kupambana na Mtibwa Sugar ya huko.

Huu ni mchezo wa kwanza wa Yanga kucheza ugenini, baada ya kupiga mechi mbili za nyumbani dhidi ya Prisons na JKT Ruvu. Hata hivyo Mtibwa Sugar nayo itakuwa kama ipo ugenini kwa vile imeamuliwa na TFF kutumia uwanja wa Jamhuri badala ya Uwanja wake wa Manungu huko Turiani katika mechi kubwa inazohusisha Simba au Yanga.

Yanga ina kibarua kigumu leo kwani Mtibwa Sugar inaundwa na wachezaji kadhaa wazoefu wa ligi hiyo ya Vodacom pamoja na michezo ya Kimataifa. Wachezaji kama Mecky Mexime, Salum Sued, Uhuru Suleiman, Shaban Nditi na Yahaya Akilimali wanatarajiwa kutoa upinzani mkali kwa Yanga ambayo imeshinda mechi zake zote mbili ilizocheza hadi sasa.

Katika mchezo mwingine wa ligi hiyo, Prisons ya Mbeya itaikaribisha Simba katika Uwanja wa Sokoine jijini humo.

Ligi hiyo inaongozwa na Kagera Sugar ambayo hadi sasa imejikusanyiia pointi 12 baada ya kushinda mechi zake zote nne hadi sasa.

Tusubiri dakika 90 za mchezo.

5 comments:

Anonymous said...

jamaa vipi matokeo huko mpira unachezwa saa ngapi?

Anonymous said...

??????????????? watakoma

CM said...

Katika mchezo wetu uliochezwa huko Morogoro, Yanga imeibuka na ushindi wa 1-0 ambalo limefungwa na Boniface Ambani.

Simba imechapwa bao 1-0.

Azam FC na Polisi Moro 0-0.

Anonymous said...

fine

Anonymous said...

saaafi saaaaaaaaaaaaaaana hiyo hata mwaka jana hawa Simba walianzia kufungwa mbeya