Wednesday, April 08, 2009

Yanga 2 Azam 3

Yanga imepoteza mchezo jioni hii dhidi ya Azam FC baada ya kufungwa 3-2 katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara uliopigwa katika Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.

Yanga ambayo tayari imechukua ubingwa, ilikuwa mbele kwa 2-0 hadi mapumziko kwa mabao yaliyofungwa na Boniface Ambani lakini ilicheza kwa ku-relax sana katika kipindi cha pili na kuifanya Azam ipachike mabao matatu.

Kipa Juma Kaseja wa Yanga leo aliokoa michomo miwili ya penati iliyoelekezwa langoni mwa Yanga baada ya timu ya Azam kupata mikwaju hiyo kutokana na wachezaji wake kufanyiwa madhambi ndani ya eneo la hatari.

No comments: