Tuesday, July 28, 2009

Ligi Kuu ya Vodacom 2009/10

Utetezi kuanzia kwa African Lyon


Shirikisho la sok nchini (TFF) limetoa ratiba ya msimu mpya wa ligi kuu ya Vodacom utakaoanza kutimua vumbi kuanzia Agosti 23 kwa vilabu vyote 12 kujitupa uwanjani huku Yanga ikianza utetezi wake dhidi ya timu ya African Lyon iliyopanda daraja.

Mechi inayosubiriwa kwa hamu na wapenzi wa soka nchini kati ya Yanga na Simba imepangwa kupigwa Oktoba 31.

Ratiba ya mechi za Yanga kwa msimu ujao ni hii hapa chini:
Raundi ya kwanza
23/08/09 - African Lyon (Dar)
29/08/09 - Manyema FC (Dar)
05/09/09 - Majimaji (Ruvuma)
08/09/09 - JKT Ruvu (Dar)
19/09/09 - Mtibwa Sugar (Morogoro)
03/10/09 - Kagera Sugar (Kagera)
07/10/09 - Toto Africa (Mwanza)
17/10/09 - Azam FC (Dar)
25/10/09 - Moro United (Dar)
31/10/09 - Simba (Dar)
08/10/09 - Prisons (Dar)

Raundi ya pili
16/01/10 - African Lyon (Dar)
24/01/10 - Manyema FC (Dar)
30/01/10 - Majimaji (Dar)
03/02/10 - JKT Ruvu (Dar)
08/02/10 - Mtibwa Sugar (Dar)
20/02/10 - Kagera Sugar (Dar)
23/02/10 - Toto Africa (Dar)
06/03/10 - Azam FC (Dar)
10/03/10 - Moro United (Dar)
14/03/10 - Simba (Dar)
27/03/10 - Prisons (Mbeya)

Kutokuwa hewani
Wapenzi wadau wa blog najua ni wengi nimewakwaza kutokana na ukosefu wa habari hapa bloguni. Hali hii ilisababishwa na mimi kuwa mbali na kituo changu cha kazi ambapo hata muda wa kutuma habari hapa ilikuwa ngumu. Ningependa kuwashukuru sana wale ambao waliendelea kutembelea blog hii licha ya kwamba hakukuwa na jipya kwa siku kadhaa lakini bila shaka link ya magazeti ya Bongo hapo pembeni ingeweza kusaidia kupata habari kuhusu klabu yetu.
Mungu ibariki Yanga.

7 comments:

Anonymous said...

pole sana ndugu na ahsante sana kwa kuanza kutupatia mapya tunakuwa na shauku kusoma habari ktk blog hii maana habari za ukweli zinapatikana hapa baadhi ya magazeti wanatuyeyusha kila la kheri

Anonymous said...

Manji katutosa kawapa viongozi changamoto ya kujitegemea.Wachezaji wanadai mwalimu anadai.Wachezaji wakigeni bado hawajaripoti kambini kwa kupewa ahadi hewa.Nilionya huko nyuma kosa la kutegemea mtu mmoja akijitoa ndio haya matatizo yake.Timu ilkuwa iende Mwanza imebaki kilabuni hamna vitanda vya maana na pesa zinadaiwa zimeliwa.

Anonymous said...

nani aliye pokea vifaa?si wam adabishe.tanzania imeendelea sisi hatutaki wabababishaji au wezi katika klabu na nchi kwa ujumla ,shikisha adabu vingozi mafisadi.

Anonymous said...

nani aliye pokea vifaa?si wam adabishe.tanzania imeendelea sisi hatutaki wabababishaji au wezi katika klabu na nchi kwa ujumla ,shikisha adabu vingozi mafisadi.

Anonymous said...

Haya sasa tutawaona, wewe unayeongelea viongozi mafisadi? mbona Kagoda huisemi? ni nani aliyefisadi?

Anonymous said...

jamani si tusubiri hizi habari zina utata, kwa mtu yeyote mwenye akili timamu, kulikuwa na maana gani kukarabati jengo na kuweka flat tv kila chumba na then mkaweke kambi mwanaza? huo si ni uhayawani na ufujaji wa pesa bila sababu? Manji yuko swa kabisa kwa hili.

Anonymous said...

mbona hiyo ratiba inatupembelea mechi zote raundi ya pili ni Dar kasoro ya mwisho tu na Prison ndio tunaenda Mbeya.