Tuesday, August 11, 2009

TFF yamrejesha Owino Jangwani...............................George Owino

Shirikisho la soka nchini TFF limemrejesha beki kutoka Kenya George Owino katika kikosi cha klabu ya Yanga kwa vile Yanga haikutangaza kumwacha katika muda uliotakiwa.

TFF ilizitaka klabu zote kuwasilisha majina ya wachezaji itakaowaacha kwa msimu ujao kabla ya Juni 30 lakini Yanga haikupeleka jina hata moja kwa madai kwamba haitaacha mchezaji hata mmoja ambaye bado ana mkataba.

Owino ambaye alisajiliwa Jangwani msimu uliopita kwa mkataba wa miaka miwili, aliachwa katika dakika za mwisho ili aende kufanya majaribio huko Ulaya ambako hata hivyo hakufanikiwa.

Yanga itabidi ikune kichwa zaidi kwani TFF imeipa siku 5 kupunguza mchezaji mmoja wa kigeni katika 6 wapya waliosajiliwa kwa ajili ya msimu ujao. Kurejeshwa kwa Owino katika kikosi hicho kunaifanya Yanga iwe na wachezaji 11 wa kigeni wakati kanuni za TFF zinataka klabu kuwa na wachezaji wa kigeni wasiozidi 10.

Wageni waliokuwepo tangu msimu uliopita ni:
  1. Obren Circkovic (Serbia)
  2. Wisdom Ndhlovu (Malawi)
  3. George Owino (Kenya)
  4. Boniface Ambani (Kenya)
  5. Mike Baraza (Kenya)

Wapya ni:

6. Joseph Shikokoti (Kenya)

7. George Njoroge (Kenya)

8. Kabongo Honore (DRC)

9. Steven Bengo (Uganda)

10. Robert Jama Mba (Cameroon)

11. Moses Odhiambo (Kenya)

Ni kusuka au kunyoa. Nani kati ya 6 mpaka 11 hapo juu atapigwa mkasi? Imekaaje hii wadau?

9 comments:

Anonymous said...

Mimi huwa sielewi hawa viongozi wetu wa TFF huwa wana matatizo gani ksbb kila mwaka wao ni lazima watuvulundie mambo fulanifulani hivi,mtu(Owino) alienda kufanya majaribio Germany na habari zikaja kuwa amefuzu sasa Yanga kama Yanga wangemjumuishaje kwenye usajili wa mwaka huu? na habari za kushindwa kwake zimekuja baada ya kipindi cha usajili kumalizika,sasa wao watalazimishaje kumrudisha kundini wakati kipindi cha usajili kilishamalizika,na wanavyong'ang'ania Yanga ikate jina la mchezaji mmoja kati ya wapya iliyowasajili mwaka huu wanategemea akishakatwa huyo mchezaji atacheza wapi wakati karibu kila sehemu vipindi vya usajili vilishamalizika?...mimi nashindwa kuwaelewa kabisa hawa watu

Tina said...

DAH MIMI IMENIUMA sana UTADHANI NDIE MCHEZAJI JAMANI,hivi Tanzania tunaenda wapi mbona soka la hapa silielewi elewi kabisa umakini hamna kabisa,hawa tff kama walitaka kuisaidia yanga si wangekataa usajili siku zote walipopeleka majina waaangalie ya zamani na wachezaji wapya baada ya kuona pingamizi limeletwa ndio wanaanza kufungua vifungu vyao ndio wanaona kuwa ni kweli.

MUGANYIZI said...

MIE NAONA HUYOMCHEZAJI OWINO AKACHEZEE VILLA YA UGANDA KWA MUDA THEN MWAKA UJAO ARUDI YANGA. VILLA IWE KAMA MARAFIKI KWA VILLE WAMETUPA BENGO.

Unknown said...

Mimi nafikiri tunahitaji TFF mpya, yenye vision ya soka la kisasa. Mambo mengi yanafanyika TFF kienyeji mno. Yenyewe inadai ina-adopt kalenda ya FIFA, requirements za FIFA na directives za FIFA. Lakini kwenye suala la usajili ni zero kabisa. Kulingana na kalenda za FIFA, timu hadi sasa zinaendelea kusajili. Na TFF wao walishamaliza usajili. Hivyo inapotokea timu za nje zinawataka wachezaji wa Tanzania basi hawawezi ku-replace. Tunatumia kanuni za kizamani katika kuendesha soka la kisasa.

Tunahitaji umakini TFF. Hakuunda kanuni mpya ila ikataka timu zitangaze wachezaji wa kuwaacha halafu kanuni baadae. Wachezaji wa Yanga wengi walienda majaribio nje (Ambani, Mwalala, Nadir, Ngasa, Owino, Mwaipopo, Nsajigwa, Obren, etc), na TFF walitaka Yanga itangaze kuacha wakati ndio kwanza wachezaji walikuwa wameondoka.

TFF inahitaji umakini na watu wa mpira wa kisasa. Na kama tuna-adopt kalenda na kanuni za FIFA basi tufanye hivyo fully, sio robo robo.

Mdau wa Yanga
Mannheim, Germany

Anonymous said...

Mechi vipi???

Anonymous said...

jamani ikiwa tim inawachezaji wakukodi zaidi ya kumi ni bora pia serikali ikakodi chama cha mpira kuongoza hapa tanzania, halaf mnasema inchi ina wasomi si bora tukajiita wapumbavu

Anonymous said...

mnavuruga mpira wa tanzania, namnakatisha tamaa vijana sijui hao wakukodi ndiyo wataleta maendeleo ya vijana hapa tanzania?

Anonymous said...

yanga 1 URA 1

Anonymous said...

timu ilikuwaje? I mean wachezaji walikuwa akina nani?