Wednesday, October 14, 2009

Kwaheri Kondic, karibu Papic

Mwezi mmoja kabla ya mkataba wa kocha wa sasa wa klabu ya Yanga Dusan Kondic kumalizika, Mserbia mwingine Kostadin "Kosta" Papic tayari ametua nchini kwa ajili ya kukinoa kikosi cha mabingwa hao watetezi.

Papic (49) alitua nchini juzi usiku na huenda akaanza kazi hiyo mara moja na endapo itakuwa hivyo, pambano lake la kwanza litakuwa Jumamosi ijayo dhidi ya Azam FC.

Papic amewahi kufundisha vilabu vikubwa vya Afrika zikiwemo Kaizer Chiefs, Orlando Pirates, Maritzburg United vya Afrika Kusini, Enyimba, Enungu Rangers, Lobi Stars na Kwara United za Nigeria.
Klabu ya mwisho kunolewa na Papic ni Hearts of Oak ya Ghana.

Papic ambaye ana leseni ya UEFA anakuwa kocha wa tatu katika mfululizo wa Waserbia kuifundisha Yanga baada Milutin Sredojevic "Micho" na Dusan Kondic.

Kazi njema Jangwani.

1 comment:

Tina said...

jamani habari za saa hizi,naombeni msisaidie maana nakosa amani moyoni nimesikia huyu kocha tuliempata zile timu alizofundisha zote alifukuzwa je ni kweli au uzushi wa wasioitakia amani jangwani ?? kama ni kweli itakuwaje sisi maana mpaka sasa tupo katika wakati mgumu,wanayanga naomba msaada wenu tafadhali nijjue