Thursday, May 27, 2010

Marekebisho ya katiba Juni 6

MKUTANO wa marekebisho ya katiba ya klabu ya Yanga, umepangwa kufanyika Juni 6 katika ukumbi wa Bwalo la Maofisa wa Polisi, Oysterbay, jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Lawrence Mwalusako, marekebisho hayo ni muhimu kabla ya uchaguzi mkuu.

Wanachama wametakiwa kwenda na kadi hai kwa maana ya kulipiwa ada na kusisitiza kuwa, atakayeshindwa kufanya hivyo, atakuwa ameikosa haki ya kushiriki mkutano.

“Uongozi unawaomba wanachama kufika kwa wingi katika mkutano huu wa kupitisha marekebisho ya katiba ya Yanga,” ilisema sehemu ya taarifa hiyo.

Kwa upande mwingine, msemaji wa klabu hiyo, Louis Sendeu, alisema kama mambo yatakwenda vizuri, mkutano huo ndiyo utapanga tarehe ya uchaguzi mkuu.

9 comments:

Anonymous said...

Huo mkutano tunaomba uwe ufumbuzi wa matatizo yote ya Yanga.

Anonymous said...

haiwezekani vingozi na baadhi ya wanachama wanafikiria kuweka hela weye mifuko yao,hakuna demokrasia ni jaja ya nyani kula embe mbichi.

Anonymous said...

kuweni wapole tu.mwisho wao unakaribia

Gray said...

ni sahihi kufanya mkutano wa kuipitia katiba na kama iko sawa kwa maslahi ya Yanga ipitishwe ili iweze kutumika kama ilivyoelekezwa na TFF. kinachoniskitisha ni jinsi muda uliotumika kuiandaa. nakuwa na mashaka na Uongozi uliopo kuwa unatumia muda mrefu katika kushughulikia suala hili kuwa una lengo la kuchelewesha kwa maslahi yao. kipindi hiki ambacho Ligi imesimama ingekuwa ni bora kufanya huo mkutano wa katiba na hatimaye tufanye uchaguzi. sasa mkutano tunafanya Juni, TFF inapelekwa lini?! nako kuna Simba kibao kwenye kamati zao. watachelewesha maksudi, halafu ipelekwe kWA MSAJILI.maana yake kuna uwezekano wa kuchelewa kufanya uchaguzi na Ligi ikaanza. nashauri Uongozi upeleke tarehe ya uchaguzi sambamba na kuwasilisha Katiba iliyopitishwa. Nina uhakika Uongozi unajua mlolongo wote huo lakini wanafanya maksudi. kwa kuwa tunataka Yanga imara na yenye Umoja, Tunaomba uongozi uhakikishe uchaguzi nafanyika mapema ili ligi ianze pakiwa na maandalizi ya kutosha kwa Timu.

Imbang permana said...

say hello
Iklan Mobil Bekas Online

Anonymous said...

Duh naona mkutano umefanyika kwa mafanikio makubwa kwa wale wanaotaka maendeleo ya yanga, aliyekuwa mwenyekiti wa yanga imani madega ametoka kwa aibu kubwa kwenye mkutano huo, akisindikizwa na polisi sijui kwa nini. Mkutano umeamua uchaguzi mkuu kufanyika tarehe 27 June 2010. Kila mwanayanga aliyekuwepo hapo alifurahia muafaka huo

Anonymous said...

Madenga kasindikizwa na polisi baada ya kumtukana
Manji.madenga alikua hataki uchaguzi ufanyike

Anonymous said...

madega huna lolote mdomo tuu,tunataka maendeleo sio mdomo .hata ukigombea kwenye uchaguzi hutapata kura yeyote .