Monday, January 24, 2011

Ligi Kuu ya Vodacom

Yanga 2 Polisi Dom 0
Yanga leo imezidi kupaa katika msimamo wa ligi kuu ya Vodacom baada ya kuichapa Polisi Dodoma kwa mabao 2-0 katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Yanga sasa inaongoza ligi hiyo kwa kujikusanyia jumla ya pointi 31 ikiwa imewaacha watani wao wa jadi Simba kwa pointi nne.

Mabao yote ya Yanga yamefungwa na mshambuliaji hatari kutoka Zambia Davies Mwape.

5 comments:

Anonymous said...

mwanzo mzuri inshaallah uzi huo huo mpaka mwisho kila la kheri kwa woote wan yanga

Anonymous said...

Yaani uongozi wa Yanga ni kiboko soma hii:
Wakati huo huo, Uongozi wa Yanga umezidi kukaliwa kooni kwa kutakiwa kufanya ukaguzi wa mahesabu baada ya kugundulika kuwa kuna baadhi ya wachezaji wamesaini mikataba miwili.

Habari ambazo Mwananchi imezipata zinasema kuwa mfadhili wa klabu hiyo Yusuf Manji ameendelea kuusisitiza uongozi chini ya Lloyd Nchunga kutaka ukagazi wa mahesabu ufanyike haraka ikiwa ni pamoja na kuwepo wa uwazi wa mapato na matumizi ndani ya klabu hiyo.

Chanzo hicho kimesema hatua hiyo imekuja baada ya kugundulika kuwa kuna baadhi ya mikataba ya wachezaji wa Yanga imechakachuliwa kwa kuandikwa miwili miwili huku ile inayopelekwa kwa mfadhili wao ikiwa na fedha nyingi.

"Unakuta mkataba aliopewa mchezaji una fedha ndogo, mfano ni Omega Seme mkataba wake ni milioni 5, lakini uliopelekwa kwa mfadhili wetu ni milioni 13, sio yeye tu wapo wachezaji wengi wamefanyiwa hivyo,"kilisema chanzo hicho.

"Nchunga (mwenyekiti) amekuwa mstari wa mbele kutaka mahesabu yakaguliwe, lakini kuna baadhi ya viongozi hawataki na ndio maana wamekuwa wakitofautiana kwenye vikao vyao vya kamati ya utendaji."

Mwaka 2008 wanachama wa klabu ya Yanga walitaka ufanyike ukaguzi wa mahesabu kufuatia shilingi milioni 150 za kadi za wanachama kutafunwa na pia shilingi bilioni 1 kutumika ndani ya siku 100 hivi karibuni kitu ambacho kinazidisha mashaka kwa viongozi wa klabu hiyo na kutakiwa kufanya ukaguzi wa mahesabu.

Anonymous said...

vingozi wengine ni majambazi tuu.. yana tuharibia wachezaji na klabu zetu,heko mr manji wewe kweli unajua unachokifanya ,wawajibike haraka wale wote waliohusika tunataka hizo hela zirudi haraka .......eti tunajiuzulu....hamna lete hesabu hizo ndio uende,

Anonymous said...

Hawa ni wakufungwa tu, hamna cha kujiuilia kazi, ni aibu iliyoje? ohh Manji anaingilia kazi? sasa yaani mchezaji ana mikataba miwili tofauti? hawa kwanza ni wakunyonga tu.

Anonymous said...

manji na wote wanaipenda yanga tunataka wale wote walioihujumu yanga kimapato waadhbiwe ,hamna cha kujiuzulu...hizo hela zirudi wezi hao.....