Monday, April 11, 2011

Ligi Kuu ya Vodacom 2010/11

YANGA BINGWA


Yanga imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya kuizamisha Toto Africa kwa mabao 3-0 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza.

Mabingwa wa zamani Simba ambayo nao walikuwa wakicheza na Majimaji na kufanikiwa kushinda 4-1 lakini ushindi huo haukutosha kuipiku Yanga kwenye mbio za ubingwa.

Yanga na Simba zote zimemaliza ligi hiyo zikiwa na pointi 49 huku Yanga ikiwa na tofauti ya magoli (Goal Difference) ya 22 wakati Simba ina 21.

Mabao ya Yanga yalifungwa katika kipindi cha pili na Nurdin Bakari(mawili) na Davis Mwape.

Inabaki kwamba Yanga ni mabingwa wa ligi ya Vodacom 2010/11.

2 comments:

Unknown said...

Mtani upo!!!!

Zile propaganda za kushikana pabaya zimeenda wapi tena?

Kateni rufaa mtashinda, TP Mazembe mliwashika pabaya na rufaa yenu itapita tu. Lazima Okwi alivuta mshiko haiwezekani akakosa penati, nawashauri kateni rufaa.

Big up Kaseja (TZ One). Umethibitisha kuwa ni golikipa bora Tz kwa kuruhusu magoli machache kabisa ambayo hayajaigharimu timu yako. Hata mmiliki wa TP Mazembe alikusifia sana.

Anonymous said...

yanga tushikamane vizuri,tumeata kocha ambaye anajua mazingara ya soka la africa.anglia papic au hata huyu mdenish wa taifa bila wachezaji bidii zao hawana lolote.