TFF yapeleka majina CAF

Wachezaji hao wapya ni pamoja na Michael Baraza aliyesajiliwa kutoka katika klabu ya RSM ya Malaysia, Ally Msigwa, Steven Marashi na Iddi Mbaga ambao walikuwa katika timu yao ya vijana.
Katibu Mkuu wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF), Fredrick Mwakalebela alisema jana kuwa majina ya wachezaji wa Yanga na Prisons itakayoshiriki mashindano ya Kombe la Shirikisho yalitumwa katika Shirikisho la soka Afrika (CAF) mwishoni mwa wiki ikiwa ni ndani ya muda uliopangwa wa kuwasilisha majina bila ya kupigwa faini.
Mwakalebela aliyataja majina ya wachezaji wengine wa Yanga watakaocheza katika mashindano hayo ya CAF kuwa ni Juma Kaseja, Nurdin Bakari, George Owino, Athumani Iddi `Chuji`, Wisdom Ndlovu, Geofrey Bonny, Castory Mumbala, Jerry Tegete, Gaudence Mwaikimba, Abubakar Ntiro, Fred Mbuna, Benard Mwalala, Shamte Ally na Mrisho Ngassa.
Wachezaji wengine ni Amir Maftah, Obren Curkovic, Shadrack Nsajigwa, Nadir Haroub 'Cannavaro', Boniface Ambani, Kigi Makassi, Hamisi Yusuph, Vicent Barnabas na Abdi Kassim' Babi'.
1 comment:
Nasikia Baraza mtambo wa magori anashuka kesho.
Post a Comment