Saturday, May 19, 2007

Sala zetu Khartoum leo


Wawakilishi pekee wa Tz katika michuano ya Kimataifa - Yanga, leo usiku itaingia uwanjani huko Khartoum kupambana na El Merreikh katika mchezo wa marudiano wa raundi ya 4 ya Kombe la Shirikisho barani Afrika.

Katika mchezo huo muhimu wa leo, Yanga inatakiwa kutotishwa na rekodi nzuri ya El Merreikh katika uwanja wake wa nyumbani na kucheza bila woga na kuhakikisha inapata sare ya magoli au ikiwezekana kushinda mechi hiyo.


Yanga inakabiliwa na matatizo ya ufungaji kwani imecheza mechi nne mfululizo za kimataifa bila ya kufunga goli hata moja. Washambuliaji akina Gaudence Mwaikimba na Saidi Maulid wanatakiwa kuwa makini katika kufumania nyavu za Wasudani hao leo.


Wana Jangwani waliweka kambi ya siku nne huko Addis Ababa na ilitua jijini Khartoum jana ikiwa na wachezaji 19 baada ya wachezaji wawili Hussein Swedi na Thomas Mourice kurejeshwa nyumbani baada ya kusumbuliwa na malaria.


Katika mchezo huo Yanga inatarajiwa kuwakilishwa na:

1. Ivo Mapunda

2. Shadrack Nsajigwa
3. Abdul Mtiro

4. Nadir Haroub

5. Wisdom Ndhlovu

6. Edwin Mukenya

7. Amir Maftah

8. Credo Mwaipopo

9. Gaudence Mwaikimba

10. Said Maulid
11. Abdi Kassim


Kama itafanikiwa kushinda, Yanga itakuwa imevunja rekodi yake isiyoridhisha dhidi ya timu zinazotoka kwenye nchi za Kiarabu.
Ni vema Watanzania tuelekeze sala zetu huko Sudan ili tuendelee kuona michuano ya Kimataifa kwa ngazi ya vilabu angalau kwa muda mrefu zaidi. Ushidi wa leo ni wa Taifa na si wa wana Yanga tu. Mungu Ibariki Yanga ya Tanzania.

12 comments:

Anonymous said...

MPAKA SASA NI GOLI 2-2, TUOMBE MUNGU DAKIKA ZIMEBAKI CHACHE MPIRA KUMALIZIKA

Anonymous said...

MPIRA UMEKWISHA TUMESONGA MBELE

Anonymous said...

Habari njema hizi

tanzanianboy said...

Lakini jamani kuna ukweli wowote hapa? Nimepita kijijini kwa Maggid kasema tumetolewa na akili yangu ilikuwa inaniambia tunatoka leo.Basi kama tumeshinda kheri sana!

Mzimba said...

Pale kijijini uzushi mwingi. Hapa ni nyumbani.

tanzanianboy said...

Masela toeni basi link tujiridhishe nafsi;maana haya mambo ya kusema tumeenda 2-2 tu bila kuambizana wapi tunaweza ona results halisi yanazidisha hofu wakubwa!

Anonymous said...

simu ya mjengwa ni hii hapa muulizeni kapata wapi matokea
255 754 678 252
labda yupo ipogolo amelewa ulanzi.

tanzanianboy said...

TUACHE KUDANGANYANA JAMANI, YANGA IMEFUNGWA 2-0 NA IMETOLEWA. MATOKEO YAKO HAPA: http://www.soccerway.com/international/africa/caf-confederation-cup/2006-2007/1-8-finals

Anonymous said...

Matokeo hayo ni mpka half time, Yanga wamefunga kipindi cha pili mpaka dk 67 goli zilikuwa 2 kwa 2

Anonymous said...

pitieni website ya caf. matokeo ni yanga imefungwa 2-0

Blatter said...

Mbona web ya fifa inaonesha 2-2?

Tenga- TFF said...

Blatter lete link kama alivyofanya tanzaniaboy, sio kubwabwaja tu kuwa web ya fifa inaonyesha 2-2

Mie najua nikuwa tumetolewa.