Saturday, September 29, 2007

Ni Wojciech Łazarek


Yanga imemtangaza raia wa Poland, Wojciech Lazarek(69) kuwa kocha mkuu wa klabu hiyo.

Lazarek ambaye kwa sasa ni mmoja wa makocha wa timu ya taifa ya vijana U23 ya Poland, anatarajiwa kutua nchini tarehe 12 mwezi ujao tayari kwa kusaini mkataba na Yanga.

Inasemekana Lazarek amewahi kufundisha pia timu ya taifa ya Sudan(2002-2004) na pia timu ya taifa ya Poland(1986-1989). Kwa upande wa vilabu amewahi kufundisha vilabu kadaa vya soka katika nchi za Uarabuni na kwao Poland.

Kuitwa kwa Lazarek kunafuatia kuondoka kwa kocha wa Yanga MserbiaMilutin Sredojevic 'Micho' katikati ya mwaka huu.

Bila shaka atamudu soka la Tz. Au sio?

No comments: