Monday, October 01, 2007

Mambo si hayo!
Wakati leo ni siku ya kusoma hitima ya baba yake mfadhili wa Yanga Yusuf Manji, mashabiki wa timu hiyo wana kila sababu ya kufurahia ushindi dhidi ya Polisi ya Dodoma wa 2-0.

Yanga ilianza ligi hiyo kwa kusuasua lakini sasa wamedhirisha kwamba wameanza rasmi ligi kwa ushindi huo dhidi wa maafande wa Dodoma.

Mabao mawili yaliyofungwa na Gaudence Mwaikimba na beki Shadrack Nsajigwa yalitosha kabisa kuwanyamazisha wale waliokuwa wakiibeza Yanga na hivi sasa wamebaki kuwa miongoni mwa timu ambazo hazijashinda mchezo wowote tangu ligi imeanza.

Sasa tujiandae na game ijayo ngumu dhidi ya maafande wa Morogoro. Tunategemea uzi utakuwa ule ule.

Alamsiki!

3 comments:

Anonymous said...

Asante sana kwa kutupasha matokeo wakati mechi ikiendelea na mara baada ya mchezo. Wale tulio mbali, tufuatilia michezo ya timu yetu kupitia blog hii.

Ubarikiwe saana, na kila la kheri Yanga Afrika.

Anonymous said...

Matokeo haya kiduchu ndiyo mmeanza kuchonga hivyo? Fanyeni kazi. Wanachama wenu wanaumia sana maana timu imetumia hela nyingi ushindi unakosekana. Timu yetu ni ya kufunga 3-0, 4-0, 5-0 style ni hiyo tu. Tupeni raha

Anonymous said...

Manchester United wametumia hela nyingi zaidi ya Yanga lakini ushindi wake ni wa 1-0 tu. Je, na wao hawafanyi kazi?