Wednesday, October 31, 2007

Mapunda, Nsajigwa miezi 6 nje
....Mukenya miezi 3
Ivo na Nsajigwa - miezi 6 nje

Kamati Kuu ya klabu ya Yanga imetoa adhabu kwa wachezaji wake waliokuwa wanatuhumiwa kutoroka kambini pamoja na masuala mengine ya utovu wa nidhamu.

Kipa Ivo Mapunda pamoja na beki Shadrack Nsajigwa wamefungiwa miezi 6 kila mmoja kutokana na kutoroka kambini, wakati mchezaji Edwin Mukenya amefungiwa miezi 3 kutokana na kuudanganya uongozi kwa njia ya simu kwamba yupo kambini wakati huo akiwa nje ya mkoa wa Morogoro.

Mshambuliaji Ben Mwalala amepewa onyo kali na uongozi wakati uamuzi kuhusu Amir Maftah umeahirishwa kutolewa kutokana na mchezaji huyo kutoonekana kwenye Kamati Kuu ya klabu hiyo.

Uamuzi huo unaibakiza Yanga na kipa mmoja tu kwa sasa - Jackson Chove, kufuatia kipa mwingine Benjamin Haule kufungiwa na TFF kwa mechi 6. Kwa sasa mshambuliaji Gula Joshua ndiye anayekaa kama kipa wa akiba katika benchi la timu hiyo.


1 comment:

Anonymous said...

Hii inahusiana na maombi ya uanachama:

http://www.mwananchi.co.tz/newsre.asp?id=2648

Hivi inawezekana kuomba tawi la wanachama wa kwenye mtandao? Yaani mheshimiwa CM anaweza kupata soft copy ya hizo application forms akaipost hapa, then wale wasioweza kufika kwenye matawi ya mtaani wakazipata hapa?

Ni pendekezo na ombi tuu...

JZah,