Tuesday, November 13, 2007

Kipa wa zamani wa Yanga aaga dunia

KIPA mahiri wa zamani wa klabu ya Yanga ya jijini Dar es Salaam, Dunia Adonis, amefariki dunia alfajiri jana katika Hospitali ya KCMC mjini Moshi alikokuwa amelazwa akisumbuliwa na matatizo ya ini.

Habari zilizopatikana jana zinasema marehemu Adonis alikuwa akisumbuliwa na ini kwa muda mrefu, ambako alikuwa akipatiwa matibabu katika hospitali hiyo hadi mauti yalipomkuta afajiri ya jana.

Mbali ya kung'ara na Yanga katikati ya miaka ya 1980, Adonis alikuwa akiichezea timu ya Veterani ya Yanga, ambako mara ya mwisho kuidakia ilikuwa mwaka jana jijini Dar es Salaam dhidi ya watani wao Simba Veterani.

Adonis ambaye alikuwa mwajiriwa wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC), pia alikuwa ni Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Soka Wilaya ya Arusha (ADFA) na mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), akiwakilisha klabu za Mkoa wa Arusha.

Marehemu ameacha mke na watoto kadhaa. Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi.

SOURCE: Tanzania Daima

1 comment:

poker said...

PROMO DELIMA
poker online terpercaya | poker online | Agen Domino | Agen Poker | Kumpulan Poker | bandar poker | Judi Poker | Judi online terpercaya | bandar qiu | situs judi online

Ayo segera daftarkan diri anda dan bergabunglah bersama kami !!
Delimapoker.com Situs Agen Poker Online Terpercaya di Indonesia akan melayani Anda dengan profesional, memproses depo/wd dgn cepat. Come join and be a winer with us !!

Untuk info selanjutnya silakan chat ke :
Livechat_____: delimapoker
BBM__________: 7B960959
Facebook_____: delimapoker
Phone number_: +85595678845
pendaftaran___