Wednesday, November 07, 2007

Msimamo wa ligi

Huu ndiyo msimamo wa ligi baada ya kumalizika kwa ngwe ya kwanza hapo jana.



P W D L F A GD PTS
1 PRISONS 13 7 3 3 20 12 8 24
2 MTIBWA SUGAR 13 6 4 3 13 10 3 22
3 YANGA 13 6 3 4 10 6 4 21
4 KAGERA SUGAR 13 5 5 3 12 12 0 20
5 TOTO AFRICA 13 5 5 3 12 10 2 20
6 POLISI MORO 13 5 4 4 11 8 3 19
7 MORO UNITED 13 3 8 2 8 7 1 17
8 JKT RUVU 13 4 5 4 11 10 1 17
9 SIMBA 13 3 7 3 11 10 1 16
10 PAN AFRICA 13 2 6 5 10 13 -3 14
11 POLISI DODOMA 13 1 9 3 13 16 -3 12
12 ASHANTI UNITED 13 2 6 5 5 13 -8 12
13 COASTAL UNION 13 3 4 6 7 11 -4 10
14 MANYEMA 13 0 9 4 5 10 -5 9

Kwa jinsi tulivyoanza ligi kwa kusuasua na mahali tulipo sasa, si haba.

4 comments:

Anonymous said...

Ni kweli, tulipo si haba kwani tulianza vibaya mno. Thank GOD, prisons wamedhibitiwa kwenye mechi za mwisho za first round. Kama timu itaingia kambini mapema na makocha wapya wakapata muda wa kuzoea timu na wachezaji kuwazoea walimu, itakuwa nzuri sana. Ni vizuri pia kama alivyopendekeza mdau mmoja, Chamangwana aendelee pamoja na makocha wapya kwa muda ili kuwa na smooth transition.

Anonymous said...

Well said Chris,
Makocha wanaweza wakawa wazuri sana lakini pia tusisahau kuna ile element ya kuwaelewa wachezaji wa kitanzania kitu ambacho nadhani Chamangwana akiwa karibu na timu anaweza akasaidia sana kuleta hiyo smooth transition.Kwa jinsi nilivyoshuhudia mimi hawa wachezaji wana uoga fulani na ujio wa hawa makocha wapya hense wanakuwa resistant kidogo ila nadhani pande zote zikijitahidi kufanya a smooth transition mambo yatakuwa sawa tu.
Tupiganie maendeleo, tuwe na timu nzuri sio timu itakayochukua tu ubingwa wa Tanzania bali pia itakayoperform well kwenye CAF club championships. Hilo la kwanza linawezekana na hilo la pili pia ila inabidi kukaza buti!!

Anonymous said...

Mimi kama ilivyopendekezwa, nakubaliana Chamangwana aendelee kubaki kwenye benchi la ufundi, ili hata hawa makocha wapya wakienda Serbia 'kwa kucheki afya' kwa muda basi timu iwe inaendelea na program zake smoothly.

Mwakani tuna mashindano ya CAF, kwa hiyo huu ni wakati mzuri wa kuiandaa timu mapema. Timu iwekwe kambini na ipatiwe mechi za kujipima nguvu na timu za nje, preferably za nchi za kiarabu kama Sudan, Egypt, Morocco, Tunisia, etc, ambazo huwa zinatupa shida tunapokutana nazo. Kama itawezekana ipelewe nje kwa mazoezi.

Uongozi uharakishe zoezi la kuingiza wanachama. Kama wataweza kuingiza wanachama 100,000 nchini kote ambao watalipa sh. 12,000 kama ada zao za mwaka, ina maana zitakusanywa sh. 1.2 billion. Hapo hakutakuwa na sababu ya kutoipeleka timu Brazil, au mahali pengine kwa mazoezi ya mwezi mzima.

Wanachama najua watakuwa willing kutoa hizi ada on time, kama wakioneshwa program inayotakiwa kutekelezwa, na utaratibu mzuri wa kukusanya kupitia benki.

Mwenyekiti Madega ameahidi kutoa program kabambe soon. Naisubiri kwa hamu!

Kila la kheri Yanga.

Anonymous said...

Kila siku wachangiaji wazuri wa mada zenye lengo la kuendeleza Yanga wanazidi kuibuka. Yaliyosemwa na brother hapo juu yana mantiki na jana habari nilizopata ni kuwa timu inapewa three weeks break then wanarudi kuanza mazoezi na huyo niliyeongea naye alionyesha kuwa Chamangwana atakuwepo pia. Program ikitoka ni wazi wanachama watakuwa willing kulipia ada zao as long as they know zitatumika ipasavyo.Tusijidanganye,ukizungumzia sums za 1bn - 2bn ni nyingi na udhibiti na transparency ya hali ya juu inahitajika kwenye hili zoezi. Ningewaomba wahasika for once waache kujifikiria wao na wajitoe muhanga kwa maendeleo ya Yanga badala yake!!!
Inshaalah, Mungu atatubariki tufike kule tunapotaka kule ambako Yanga inastahili kufika na huko ni kuwa moja ya timu bora kabisa Afrika na labda siku moja soon kuwa na uwezo wa kuwaalika Liverpool tuwapige bao 8 kama wao walivyowapiga Beskitas!!