Saturday, November 03, 2007

Tumalizie na Manyema FC

Ile kazi iliyokuwa imeanza hivi karibuni ya vijana wetu kuonyesha kandanda safi inatarajiwa kuendelea tena kesho kwa pambano la mwisho la kumalizia ngwe ya kwanza ya Ligi Kuu ya Vodacom kwa kucheza na Manyema FC katika Uwanja wa Jamhuri huko Morogoro.

Manyema ambao ni "mabingwa wa kutoa sare" wanatarajiwa kukutana na Yanga ambayo imeanza kucheza mpira wa uhakika kiasi cha kuwarejeshea furaha mashabiki wake baada ya kutaabika kwa muda mrefu.

Yanga itaendelea kuwakosa wachezaji wake kadhaa lakini kama ilivyokuwa katika mechi iliyopita dhidi ya Prisons, hakuna pengo litakaloonekana kufuatia kandanda safi lililoonyeshwa na vijana hao wa Jangwani chini ya kocha wao Jack Chamangwana.

Pambano hili pia huenda likawa la mwisho kwa Jack Chamangwana kama kocha mkuu endapo uongozi wa klabu hiyo utaingia mkataba na makocha wawili kutoka Serbia ambao wapo nchini tayari kwa kujiunga na Yanga.

Tunawatakia kila la heri wachezaji na mashabiki wote.

Kwa wale wafuatiliaji wa mechi hii wanaweza kuungana nami hapo chini katika comments kujua kile kinachoendelea uwanjani. (endapo mawasiliano yatakuwa mazuri)

8 comments:

Anonymous said...

Kila la kheri vajana. Bila shaka tutamaliza ngwe hii ya kwanza katika nafasi ya pili. Yanga mbele daima.

Anonymous said...

Nafasi ya pili kwa ngwe hii yaweza kuwa ngumu but Inshaalah!Mwenyezi Mungu atajaalia the cup might be ours come the end of the next round! Yanga daima mbele!!

Anonymous said...

Tusijidanganye bado mambo sana.Timu niliyoiona Mbeya inahitaji marekebisho makubwa sana.Kwa sasa hatuna kocha kwani Chamangwana mtupu.Ushindi ulitokana na juhudi za wachezaji wenyewe.Pia wachezaji wengi niliongea nao wamesema kwamba Ivo na Nsajigwa wameonewa.Viongozi wanakumbatia wachezaji wageni ndio maana Mukenya amepewa adhabu ndogo zaidi kwa kutoroka kambini tena kabla ya pambano na Simba.Huku wengi wakimtuhumu kwamba ana mawasiliano na Simba.

Anonymous said...

Mpira sasa ni mapumziko. Tunaongoza bao 1 ambalo Manyema wamejifunga wenyewe

Anonymous said...

Mpira umekwisha. Matokeo ni 1-0, sasa tumemaliza ngwe ya kwanza na pointi zetu 21.

Leo wadau mmekuwa kimya sana. J'pili njema!

Anonymous said...

Nashukuru sana kwa matokeo cm. wakati tunatafuta ni wapi tulipojikwaa, point 21 si haba. Yanga daima mbele.

Anonymous said...

Nashukuru sana kwa matokeo cm. wakati tunatafuta ni wapi tulipojikwaa, point 21 si haba. Yanga daima mbele.

Anonymous said...

Tulipomalizia sio pabaya, turekebishe makosa tusonge mbele.
Napenda nitofautiane na mdau anayesema Chamangwana mtupu,pengine hii inatokana na kutaka kuulinganisha mpira wetu huu na mpira anauona kwenye TV wa akina Man U,Arsenal n.k
Ukweli utabaki kuwa Chamangwana is good at getting results although the team may not play entertaining football but we do get the results tukiachana na mechi za Simba ambazo kila mwanayanga anajiuliza huwa tunajikwaa wapi.Hao wachezaji mdau anaowasifu wanaweza kufanya vema zaidi kama sio kuelemewa na starehe na kama ulikuwepo kweli Mbeya utakubaliana na mimi kwamba meza moja pale Mbeya carnival ilikuwa na wachezaji takribani 6 wa Yanga waliocheza siku ile na walikula mitungi mpaka saa 9 usiku!!
Mimi pia nilibahatika kuongea na baadhi ya wachezaji na hata coaching staff,hao jamaa wawili wala hawajaonewa na baadhi wanadhani bila adhabu zile nidhamu kwenye timu ingepotea na kiini cha adhabu zile ni mambo ya ndani zaidi na sio haya yanayosemwa kwenye magazeti.
Kwa ujumla nadhani tuuangalie mpira wa vijana na tukubali kuwa mpira unaochezwa sasa hivi una tofauti na wa mechi za mwanzo though ushindi sio wa uhakika sana na wa magoli mengi lakini pia tumekuwa solid na hatufungiki kirahisi.Hakuna wachezaji ambao wana maisha ya kudumu Yanga,Ivo na Nsajigwa wanapaswa kuwauliza watu kama Denis Mdoe au Said Swedi nini kiliwakuta Yanga.Walau Ivo amekiri kosa na kujutia,maneno anayotoa Nsajigwa hasa kwenye press yanaonyesha level yake ya commitment to Yanga F.C