Friday, December 28, 2007

Akina Ivo kusamehewa leo?

Kamati ya Utendaji ya klabu ya Yanga leo inatarajiwa kukutana kujadiliana mambo mbalimbali kuhusu klabu hiyo.

Wadadisi wa mambo wanasema huenda suala la kufungiwa akina Ivo Mapunda likajadiliwa.

Wakati huo huo kuna habari kuwa Yanga inajiandaa kucheza michezo kadhaa ya kirafiki huko Afrika ya Kusini. Hata hivyo pamoja na vyombo kadhaa vya habari kudai kwamba itacheza kesho na Kaizer Chiefs, tovuti ya klabu hiyo inaonyesha kwamba timu hiyo haipo kambini mpaka tarehe 5 Januari. Tutaendelea kufuatilia habari hii.

Wadau mnisamehe leo computer ina matatizo kidogo ya kiufundi, siwezi ku-format habari.

4 comments:

Anonymous said...

Inabidi wapewe msamaha mapema ili waungane na wenzao haraka. Hii itamsaidia kocha kufikiria na kuandaa first 11 kwa ajili ya michuano ijayo.
wenzetu wanatumia neno 'to jell'
-it takes time for players to jell.
Kwa hiyo uongozi Yanga wasijipe matatizo ya baadaye kwa wachezaji kutokuelewana maana hili liko mikononi mwao! Wachezaji huelewana vema wanapokuwa pamoja kambini kwa muda wa kutosha - hii itasaidia washambuliaji kuelewana na hivyo kufunga magoli na idara nyinginezo kama viungo na walinzi katika kuzuia mashambulizi ya wapinzani na kuisaidia safu ya washambuliaji. Matokeo yake ni ushindi wa timu, mashabiki nasi tunaburudika!

Yanga Imara zaidi 2008.
Kila la heri 2008

-mdau Berks, UK

Anonymous said...

Kwa sababu zisizoweza kuzuilika, kikao hakikufanyika mpaka baada ya mwaka mpya.

Kwa hali hiyo basi, Ivo na Nsajigwa wataendelea kusota nje ya uwanja.

Anonymous said...

Mwalala nae yupo Afrika Kusini licha ya kuchelewa kambini.Eti amewekwa kiporo!!!Hivi dhambi gani kubwa hasa waliofanya Ivo na Nsajigwa???Kuna kitu kinafichwa.Kwanini Mwalala aruhusiwe kuwa kule na hafanyi mazoezi???Kwanini Yanga tunalea uzembe???

Anonymous said...

Wote ni wakosaji tu tena huyo Mwalale wenu ndiyo ana matatizo makubwa zaidi. Wachezaji wote duniani wanajulikana kwa kuwa na matatizo mengi. Ni jambo la busara kwa wapenzi na kwa wachezaji pia kuwa msamaha huu utaleta mshikamano zaidi kuliko utengano.

Think twice ndugu zangu Yanga inatakiwa isonge mbele na itatokana na uimara na ushirikiano wa wachezaji na viongozi wote.

Baba Kelvin wa Temboni