Tuesday, December 18, 2007

Kikosi kuondoka leo

Kikosi cha wachezaji 20 wa klabu ya Yanga kinatarajiwa kuondoka leo kuelekea nchini Afrika ya Kusini kwa ajili ya kuweka kambi ya mazoezi kwa muda wa wiki tatu

Yanga inaondoka na kikosi chake kilekile kilichokuwa kinafanya mazoezi huko Mwanza kwa muda wa wiki mbili chini ya kocha Dusan Kondic.

Wachezaji waliokuwa katika timu zao za Taifa katika michuano ya Challenge, wachezaji waliofungiwa pamoja na Ben Mwalala wameachwa katika safari hiyo.

Wachezaji walio katika timu za taifa ni Vincent Barnabas, Amiri Maftah, Castory Mumbala, Abdi Kassim na Nadir Haroub. Wachezaji waliofungiwa ni Ivo Mapunda na Shadrack Nsajigwa. Pia wachezaji Ben Mwalala licha ya kutua Dar ameachwa katika safari hiyo pamoja na Said Maulid SMG ambaye ameingia mkataba na timu ya Bravo du Marquiz ya Angola.

Tunawatakia safari njema, mrudi mkiwa mmeiva kisoka.

1 comment:

Anonymous said...

Siku za karibuni kumekuwa na tabia ya kusajiri wachezaji wa kutoka Kenya. Ni wachezaji wazuri na kwa kweli wanakiwango kizuri cha kusajiriwa Yanga.

Tumeshuhudia mara nyingi kuwa Wakenya wote Wanaenda kwao mara kwa mara aidha wanapoitwa kwenye timu zao za taifa (kwa kuwa ni wakali, mara kwa mara wanaitwa) au "KWENDA KWENYE MATATIZO YA KIFAMILIA" (Wanaonekana wana matatizo ya kifamilia zaidi kuliko Watanzania). Inakela sana maana ukifanya tathmini utagundua kuwa Wakenya wana muda mfupi sana wa kuchezea timu yetu kuliko wenzao Watanzania. Tumeona kwa Mukenya, Mwalala, Sunguti naye. (Simba nao wamewahi kupata matatizo hayohayo)

Hapo kwa Mwalala ndiyo viongozi walichemsha kabisa. Kumsajiri mtu ambaye tulikuwa na matatizo naye kwa msimu mzima na ambaye hatukuona faida yake. Mwalala ni mzuri lakini kama hachezi uzuri wake unakuwa wapi?

Mimi nawaomba viongozi wetu waachane na hao WAKENYA maana hakuna faida yoyote timu inapata kutoka kwao licha ya kupata mishahara mikubwa, nyumba, kulipiwa uhamiaji na gharama nyingine nyingi sana. Sajilini Watanzania mtapata raha na kusaidia watanzania wenzenu.

YANGA DAIMA MBELE.......