Thursday, December 13, 2007

Kondic aelekea Sauzi

Kocha Mkuu wa klabu ya Yanga Dunsan Kondic leo anatarijia kuondoka nchini kuelekea huko Afrika Kusini kwa ajili ya maandalizi ya kambi ya timu hiyo itakayopigwa nchini humo hivi karibuni. Yanga ambayo inajiandaa na michuano ya mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara pamoja na michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika, kwa takriban wiki mbili sasa imeweka kambi huko Mwanza kujifua na michuano hiyo.

Mwalala siku 3 hizo
Wakati huo huo sakata la mchezaji limeingia katika khatua nyingine, baada ya uongozi wa klabu hiyo kumpa siku 3 awe amerejea la sivyo itamchukulia hatua za kisheria kwa vile kutokuwepo kwake ni kukiuka mkataba.

9 comments:

Anonymous said...

Nilichogundua kwa Mwalala ni kwamba jamaa ni mvivu wa mazoezi hasa kama kuna usimamizi wa kutosha.

Ikumbukwe kwamba Mwalala huyu huyu alishindwa kuelewana na Micho kutokana na kocha huyo kusimamia ipasavyo mazoezi. Wakati wa Chamangwana, aliweza kucheza kwa vile makocha wengi wa kiafrika wana-tolerate visababu vidogo vya wachezaji mara kichwa kinauma, mara mgongo, mara tumbo ili mradi asifanye mazoezi magumu.

Anonymous said...

Amekacha kambi karibu mwezi wa pili.Madega anadai hapokei simu.Sasa siku 3 za nini??Atimuliwe tusajili wachezaji wenye nia na mapenzi ya kuchezea Yamga.

Anonymous said...

Ndugu wadau mshambuliaji wetu Said Maulid SMG ameingia mkataba wa mwaka 1 na klabu ya Bravo Marquiz ya Angola.

Yanga tayari imeridhia uhamisho huo.

Kila la heri SMG.

Anonymous said...

Kila la kheri SMG. Ameitumikia Yanga kwa moyo wote na nidhamu tangu atoke kwa watani, licha ya matatizo yaliyoambatana na uamisho wake. Huo uwe mano kwa wachezaji wengine.

Mungu ambariki huko aendako.

JM.

Anonymous said...

Kwa habari za kiufundi za soka tembelea www.tuntucoach.blogspot.com

Anonymous said...

Mwlala Mwalala siku 3 zitapita viongozi watatumwa mtu kumbembeleza.Keshatangaza wazi kwamba harudi Yanga tunambembelezea nini???

Anonymous said...

Sioni sababu ya kumbembeleza Mwalala. He is not the best player he thinks he is. Mchezaji kama Wisdom Ndlovu, ni wa kiwango cha juu kuliko Mwalala, lakini husikii hata siku moja akileta maringo.

Pia nadhani tufanye evaluation, tumefaidika vipi na hawachezaji wa nje in the past 5 years. Na je tunahitaji kuendelea kutafuta wengine? Nafikiri wachezaji wa East Africa (Kenya na Uganda hasa) wana tabia fulani zinazofanana (za utapeli). Ni wasumbufu. Mifano iko wazi: Mwalala, Mukenya, Denis Onyango..., huenda na wachezaji wetu wakienda nje wako hivyo pia.

Ni wakati wa kuweka nguvu kwenye timu yetu wa vijana. Badala ya kutumia 20M KUMSAJILI MSUMBUFU MMOJA asiyejua hata umuhimu anaopewa, ni afadhili hizo hela ziende kuendeleza timu ya vijana, ipelekwe nje kwa mafunzo, na ipatiwe vifaa vinavyotakiwa. Investment kama hiyo ina long term returns kwa Yanga Taifa, kuliko kina Mwalala.

Hata akirudi ningependekezwa apewe adhabu kama ya kina Ivo, kwanza arekebishe tabia yake!

Anonymous said...

Nani anajua kama amerudi au la??Aumviongozi wameamua kufunika kombe mwanaharamu apite??Kama hakuna lililotokea.

Anonymous said...

Nani alikwambia yanga tunafanya usajili? Sisi siku zote tunazoazoa tu. ndio maana watu kama akina mwalala wanapeta maana wanajua ni muda gani waje wachukue pesa na muda gani waende zao.

Tuanza mpango wa kuwaona wachezaji mapema na kuwafatilia kabla ya kusajili. Tuache zima moto!!