Monday, December 10, 2007

Mwalala aanza tena mambo
Mshambuliaji nguli wa Yanga kutoka Kenya Ben Mwalala bado mpaka sasa hajaripoti kambini na hivi sasa yupo kwao Kenya.

Mwalala ambaye miaka ya nyuma alikuwa akichomoka mara kwa mara kwenda kwao Kenya na kuchelewa kurudi kambini, inasemekana yupo huko kwa matatizo ya kifamilia ingawa habari ambazo hazijathibitishwa zinasema kwamba Mwalala ameuwekea ngumu uongozi wa klabu hiyo kufuatia kutomaliziwa fedha alizoahidiwa na klabu hiyo.

Yanga hivi sasa ipo kambini huko Mwanza chini ya kocha Dusan Kondic.


4 comments:

Anonymous said...

Naomba kuuliza, ni kwanini Yanga ktk michuano ya klabu bingwa Afrika msimu uliopita ilicheza mechi moja tu U/Taifa na haikwenda ugenini kwenye mechi ya marudiano? Nadhani ilicheza na timu toka Komoro na kushinda 5-1 u/Taifa!

Anonymous said...

Nilisema hapo nyuma kuhusu Mwalala na mtoaji maoni mmojawapo akamtetea kwamba uongozi unajua matatizo yake.Mwalala ni mbabaishaji tu.Viongozi wanamlinda wakati sio mchezaji wa kutisha na hana faida kwa Yanga.Ikiwa tunataka kujenga timu imara basi tuache ubaguzi Ivo na Nsajigwa wameadhibiwa vikali kwanini Mwalala anadekezwa.Au kuna makundi ya wachezaji Yanga????

CM said...

Anon wa kwanza hapo juu ni kweli kwamba Yanga ilicheza mechi moja tu na timu ya AGSM kutoka Comoro kwa vile nchi hiyo haikuwa na Uwanja unaokubalika na CAF.Kwa hiyo iliamuliwa icheze mechi moja tu.

Katika mechi hiyo iliyofanyika katika Uwanja wa Taifa, Yanga ilishinda 5-1.

Anonymous said...

Huyu jamaa ni mchezaji mzuri lakini kama haya mapozi yake yanaendelea, ni bora naye aitwe ajieleze.

Ni bora tubakiwe na akina Barnabas, Tegete nk kuliko kuendelea kumdekeza huyu jamaa.