Wednesday, December 19, 2007

Mwonekano mpya wa Amir Maftah

Amir Maftah katika mwonekano wa zamani(kushoto)
na wa sasa(kulia)

Leo sina habari nzito sana, ila nina habari nyepesi inayomhusu beki wa timu ya Kilimanjaro Stars na Yanga - Amir Maftah. Kama anavyoonekana pichani juu, ni kwamba ameamua kuondokana na rasta hivyo kwa wale mashabiki ambao walikuwa wakimtambua kutokana na nywele zake itabidi watafute utambulisho mwingine wa haraka.

Inasemekana Kocha Mkuu wa Kilimanjaro Stars Marcio Maximo amewataka wachezaji hao kuondokana na kuwa na nywele ndefu wanapokuwa katika timu ya Taifa.

Ningependa kutumia nafasi hii pia kuwashukuru wadau wote kwa kutembelea blog hii pamoja na wale wanaotoa maoni yao katika habari mbalimbali hapa bloguni.

Daima tupo pamoja!

6 comments:

Anonymous said...

Naomba uandike listi ya wachezaji wa Yanga na positions zao! Mimi majina nayaona lakini nafasi zao sizijui. Niko Uingereza!

Pia andaa mada tujadili wachezaji wa zamani kina Juma Mkambi -Jenerali!!!

Anonymous said...

Orodha ya wachezaji wa zamani Yanga ambao ni hazina na mfano wa kuigwa kwa wachezaji wa sasa! Wachezaji wa leo hawajafikia kiwango ambacho tulikiona kwa hawa nyota wa zamani.
Inabidi uongozi wa timu ujiulize ni nini tumekikosa Yanga hadi kiwango na ubora wa kikosi chetu umeshuka kiasi hiki?

Rashid Hanzuruni -mshambuliaji,
Omari Hussein -mshambuliaji,
Makumbi Juma 'hama ya jiji'-mshambuliaji,
Athuman Juma Chama -mlinzi,
Juma Shaaban -mlinzi,
Allan Shomari -mlinzi,
Hamis Kinye -GK
Joseph Fungo -GK
Juma Pondamali -GK
Isaack Mwakatika -kiungo
Ahmed Amasha -mlinzi
Charles Boniface -kiungo
Charles Kilinda -kiungo
Charles Alberto -kiungo
Edgar Fongo -mshambuliaji
Abedi Mziba -mshambuliaji
Fred Felix Minziro 'majeshi' -mlinzi
Athuman China -kiungo
Saidi Mwamba 'Kizota' -kiungo/mshambuliaji
Edibily Lunyamila -kiungo
Saidi Mrisho 'ziko wa kilosa' -mshambuliaji
Juma Mkambi 'jenerali' -kiungo
Constantin Kimanda -mlinzi
Ngandu Ramadhani -mlinzi
Yusufu Macho -kiungo
Sekilojo Chambua -kiungo
Saidi Suedi 'scud' -mshambuliaji

n.k.
Kwa kweli hawa wachezaji enzi zao waliiwakilisha Yanga kwa moyo na matunda tuliyaona. Nakumbuka Yanga ilitwaa ubingwa Bara 1981, 83, 85, 87, 89? na pia Muungano pamoja na kuzifunga Simba na Pan African!

Nawaomba washika dau wote Yanga tuzungumze na kutafuta dawa muafaka ili kurudisha heshima ya enzi hizo!

Anonymous said...

Samahani kuna baadhi ya wachezaji wa muhimu sana nimewasahau. Hii haina maana kuwa hawakuwa na mchango wa kukumbukwa; ila ni kumbukumbu zangu ndio zimeniangusha!
Wote nawatambua na kuthamini mchango wao!
Nachoomba ni wachezaji wa sasa kuiga na kufuata nyayo ili Yanga ing'ae tena.

Anonymous said...

Salum Kabuda Ninja -mlinzi
Salvatory Edward -kiungo
Kenneth Mkapa -mlinzi

CM said...

Anon wa kwanza - Kikosi cha sasa cha Yanga na positions zao unaweza kukipata endapo uta-click link ya "KLABU YETU" hapo pembeni.

Unknown said...

jamani mmemsahau nonda shaban papii tena huyu asitueleze kitu chochote kaanzia black star na watoto wenzie kipindi hicho.