Thursday, January 17, 2008

Hatma ya akina Maftah kesho
Amir Matah

Kamati ya Nidhamu ya klabu ya Yanga inatarajiwa kuketi kesho kujadili miongoni mwa mambo mengine ni suala lililowekwa kiporo la kutoonekana kambini kwa wachezaji Amir Maftah pamoja na Ben Mwalala.

Maftah anakabiliwa na tuhuma za kuondoka kambini baada ya mchezo wao dhidi ya Simba uliofanyika Oktoba 24 mwaka jana huko Morogoro. Maftah alitoroka pamoja na Ivo Mapunda na Shadrack Nsajigwa ambao tayari wamefungiwa miezi sita kwa kosa hilo. Maftah hakuwepo katika kikao kilichowafungia akina Ivo hivyo suala lake liliwekwa kiporo.

Naye Ben Mwalala anatakiwa kujieleza ni kwanini alishindwa kujiunga na kambi ya klabu hiyo mapema.

Wakati huo huo, Yanga haitampa mkataba mpya Kocha wa zamani wa makipa Razak Siwa. Siwa pamoja na Jack Chamangwana walikuwa na jukumu la kuandaa timu ya vijana ya Yanga.

2 comments:

Anonymous said...

Kamati imeshindwa kukaa kutokana na wajumbe wengi kuwa na udhuru hivyo suala la wachezaji hawa linaendelea kubaki kiporo

Anonymous said...

Mwalala hataadhibiwa analindwa na viongozi.Hawana uwezo wa kumuadhibu.Hata afanye nini watavumilia tu.Maftah anaponea hapo.Ingekuwa yeye yupo peke yake angeshafungiwa siku nyingi.Kwani hawakujua kwamba Kisasa atakuwa safarini walipokuwa wanatayarisha kikao??WAACHE LONGOLONGO.