Monday, January 07, 2008

Makali ya "Bondeni" kuonekana leo

TIMU ya Yanga leo usiku inatarajia kujitupa uwanjani kuumana na timu ya Polisi ya Zanzibar kuwania Kombe la Mapinduzi mchezo unaotarajiwa kufanyika Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Michuano hiyo iliyoanza jana inashirikisha timu za Polisi Zanzibar, Duma, Miembeni na Jamhuri kwa upande wa Zanzibar wakati Bara ni Yanga na Mtibwa Sugar.

Yanga inatarajia kuonesha cheche katika mchezo huo, baada ya kurejea nchini juzi ikitokea Afrika Kusini ilikokuwa kwa wiki kadhaa katika mafunzo.

Timu hiyo iliweka kambi nchini humo takribani wiki tatu kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara na michuano ya Kombe la Shirikisho.

Timu hiyo inayonolewa na kocha wake Dusan Kondic, ilicheza michezo minne ya kirafiki na kushinda miwili na kutoka sare miwili.

MAJIRA

6 comments:

Anonymous said...

Tumechapwa 3-2.

Asanteni

Anonymous said...

Wachezaji walitamba kwamba Simba kawaogopa na kuacha kuwa makini.Mpaka hapo wachezaji wetu watakapoaacha kujitapa na kucheza mpira kwenye magazeti basi tutaendelea kufanya vibaya,Nashauri uongozi wawazuie wachezaji kuropoka ovyo kwenye magazeti chezeni mpira ndio kazi yenu.Kazi ya kuongea na magazeti waachieni wanaohusika.Ni aibu kufungwa na Polisi pamoja na mazoezi ya muda mrefu na kupewa kila kitu.Inawezekana hatuna aina ya wachezaji tunaowahitaji bali mabishoo na wapenda sifa.Chezeni mpira mnapewa kila kitu.Inauma sana.

Anonymous said...

Nakubaliana na wewe.Wachezaji wetu wanaongea sana.Mbuna walipotua Airport kaanza kujitapa ohh hakuna timu ya kututisha.MATOKEO TUMEFUNGWA NA VIBONDE.Waache ngebe wacheze mpira.

Anonymous said...

Madega naye akihojiwa baada ya mchezo alisema kwamba stamina za wachezaji zipo juu.Na kadiri mpira ulikuwa unaendelea ndio stamina zao zilizidi!!!!!Hakuna kimube wa namna hiyo.Mchezaji yeyote huwa anachoka kadiri mpira unavyokwenda ila level ya kuchoka inategemea na stamina uliyonayo.Watu wa namna hii wanaozungumza utumbo ndio tumewachagua kuongoza Yanga.Yeye sio kocha nani kampa right ya kuongelea mechi?Kazi hiyo ni ya kocha na yeye ndio mtaalamu.Madega just shut up.

Anonymous said...

Makali yepi??Ovyo utumbo mtupu wanatia hasira.

Anonymous said...

Wachezaji wameanza kulalamika kwamba viwanja huko Bondeni vilikuwa vibovu-Surprise!!!Eti pia walicheza na timu za wapishi na mateksi dereva!!!Kweli hayo ndio mazoezi tuliokuwa tunasifiwa.Waliona mechi na Polisi wanasema timu ilicheza mchezo mbovu kupindukia.Huku kocha akilalamika kwamba kambi imekatishwa kwa mashindano ambayo yasingetuongezea lolote.Kwa viongozi hawa ikpo kazi.