Thursday, January 10, 2008

Mazoezi ya Sauzi:
Yanayosemwa ni majungu au ya kweli?


Licha ya viongozi wa Yanga kujivunia kambi iliyowekwa na klabu hiyo huko Afrika Kusini, inaonekana kwamba kambi hiyo ilikuwa na mengi kutoka kwa wachezaji.

Inasemekana pia kocha mkuu wa timu hiyo Dusan Kondic alipokuwa Afrika Kusini alichagua makundi matatu, la kwanza la wachezaji waelewa, la pili waelewa lakini wanahitaji muda mwingi wa kufundishwa na la tatu kiwango chao kisoka kimefika mwisho hawafundishiki kabisa.

Aidha kwa mujibu wa baadhi ya wachezaji, viwanja walivyokuwa wanafanyia mazoezi huko Afrika Kusini vilikuwa vibovu hivyo kuwachosha na kushindwa kushika vizuri mafunzo ya makocha wao.

Pia imeelezwa kwamba timu walizocheza nazo mechi za mazoezi hazikuwa timu za kimashindano, kwani timu nyingine walizocheza nazo zilikuwa ni za madereva wa teksi pamoja na wapishi.

Haya ndugu wadau kama hizi habari ni za kweli basi hali ya mambo kwenye timu yetu si shwari. Tuombe usalama tu.


1 comment:

Anonymous said...

UKWELI KWAMBA WALICHEZA NA TIMU ZA MADEREVA TEKSI NA WAPISHI???Kwanza hebu angalia viongozi wanavyotofautiana.Madega alisema wachezaji wana stamina na inazidi kuongezeka mpira ulivyokuwa unaendelea na Polisi (sic)Kisasa naye kakurupuka na kusema tulifungwa kwa sababu ya uchovu ikipingana na kauli ya Madega.Francis Lucas nae kaja na mpya eti kuna makundi matatu kama ulivyotaja hapo juu naeti kundi la wasiofundishika eti anahisi wamejijua ndio maana wanaeneza majungu.Ohh please.Waliambiwa hawafundishiki na yeye Lucas anawajua???Kama ni kweli kwanini bado wapo Yanga???Tairi limebasti na haliwezi kutengenezwa unaweka kwenye buti la nini???Lucas kama ni kweli kambi ya Afrika Kusini ilikuwa mbovu basi kuna haya ya kusema ukweli na siyo kutumia visingizio na vitisho.Uwezo wa viongozi wetu kuongoza ni dhaifu sana kwani kila moja anasema lake.Nani ndio spokesman wa timu na klabu kwa jumla??