Wednesday, January 16, 2008

Ukombozi ni mpaka April 27

Mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom inatarajiwa kuanza 26 Januari kwa timu ya Yanga kufungua dimba na Ashanti United katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam. Hata hivyo pambano linalosubiriwa kwa hamu kati ya Simba na Yanga litapigwa Aprili 27.

Ligi hiyo inatarajiwa kumalizika siku hiyo ya Aprili 27 na siku hiyo inatarajiwa kuwa siku ya 'ukombozi' kwa timu ya Yanga kwani haijaifunga Simba kwa zaidi ya miaka 4.

Prisons inaongoza ligi hiyo ikiwa imejikusanyia pointi 24 kutokana na michezo 13 iliyocheza, ikifuatiwa na Mtibwa pointi 22, Yanga inashika nafasi ya tatu kwa pointi 21, wakati miamba wengine, Simba wamejikusanyia pointi 16 katika mzunguko wa kwanza.

Ligi hiyo itamalizika mapema ili kutoa nafasi kwa timu ya taifa kuanza kambi kwa ajili ya kujiandaa na michuano ya kufuzu kushiriki michuano ya fainali za Kombe la Dunia za mwaka 2010 zitakazofanyika Afrika Kusini na ile ya michuano ya Mataifa ya Afrika itakayofanyika Angola mwaka huohuo.

Kazi kwetu.

4 comments:

Anonymous said...

Tuache kujitapa.Na kutumia maneno kama ukombozi.Mara ya mwishi tulifungwa kwa kutangaza kwamba tuna milioni 50.
Leo katika mahojiano na waandishi wa habari Kocha wetu kasema timu yetu ina mapungufu mengi hivyo tuache kutamba na kukamia mechi moja.Tujenge timu na mafanikio yatakuja na mafanikio sio kumfunga Simba bali timu inayocheza mpira wa kisasa na kueleweka.Ushabiki wa kwenye kahawa tuache.Tukae kimya tufanye mambo yetu kistaarabu na mafanikio yatakuja.

Anonymous said...

Ukombozi kwani sasa tupo utumwani???Tusipime mafanikio ya timu kwa kuifunga Simba.Lazima tuwe na mawazo ya kuangalia mbele zaidi.Pamoja na kwamba Simba ni wapinzani wetu wa jadi lakini tusiwekeze nguvu zetu zote kwa timu moja bali lengo liwe ni kuchukua ubingwa na kufanya vizuri kwenye kombe la shirikisho.

Anonymous said...

Pamoja na mafanikio yote tunaweza kuyapata lakini tutajihisi upungufu kama tutaendelea kuwa wateja wa Simba kwa miaka yote hii.

Hivyo neno "UKOMBOZI" limetumika kama kionjo tu.

Anonymous said...

Inferiority complex hiyo.Tuache majungu tujenge timu.Kufungwa ni kufungwa tu.Ndio maana mpaka leo Ivo na Nsajigwa wanawekewa mikwara kwa uvumi usiokuwa na maana yeyote.Kuwafungia wachezaji miezi sita kwa kuondoka wakihofia usalama wao ni ujinga mtupu.Labda tuambiwe walifanya kosa lingine.Kuna madai kwamba walicheza chini ya kiwango!!!Sijui nani ali monitor hicho kiwango.Washambuliaji wetu walishindwa kabisa kufunga goli licha ya Simba kucheza 10 kwa dakika 74.Na wao pia washukiwe???Tutaacha lini mpira wa chuki???