Saturday, January 12, 2008

Yanga yaanza kujipima leo

Wawakilishi wa Tanzania Bara katika michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika, Yanga leo wanaingia katika Uwanja wa Taifa Jijini Dae kupambana na Ashanti United katika mchezo wa kujipima nguvu.

Yanga iliyokuwa kambini huko Afrika ya Kusini, leo inatarajiwa kuwaonyesha hasa kile walichokuwa wanakifanya huko 'bondeni' kwani mashabiki wengi hasa wa Dar wamechoshwa na sifa zinazopamba magazeti kila kukicha kuhusu kubadilika kwa kikosi cha Yanga wakati matokeo ya hivi karibuni ya Kombe la Mapinduzi yameleta shaka juu ya habari hizo.

Wakati huo huo, mshambuliaji Ben Mwalala yupo katika kikosi cha timu hiyo akiendelea na mazoezi pamoja na wachezaji wenzake. Inasemekana uongozi wa timu hiyo umemweka kiporo mchezaji huyo hadi hapo Kamati ya Utendaji itakapokaa.

8 comments:

Anonymous said...

Wadau nipo uwanjani. Hivi sasa ni mapumziko. Bado ni 0-0.

Kwa kweli naona mambo bado. Tusubiri 2nd half

Anonymous said...

Tumeshinda 2-0. Wafungaji ni Sunguti na Abuu Ramadhani.

Dakika za mwisho Yanga wameweza kuonyesha uwezo wao vizuri. Labda Madega alikuwa sahihi huko Zenji.

Anonymous said...

wacha kuficha ficha sema kweli timu ilkuwaje??imebadilika??Kuishinda Ashanti huwa tunashinda mara kwam mara.Cha maana wachezaji wanaonekana kubadilika???

Anonymous said...

Hivi tatizo ni nini? wachezaji wanakaa kambini mwezi mmoja wanifunga Ashanti goli 2? je wasingekaa kambini?

Anonymous said...

Muhimu i uchezaji watimu. Sio lazima kuiunga Ashanti goli 10 ndo timu iwe imekamilika. Ashanti nayo ni timu na imejiandaa kama Yanga ilivyojiandaa. Tuangalie uchezaji wa timu nzima, sio matokeo tuu.

Anonymous said...

Madega amekaririrwa akisema kwamba timu yetu haiwezi kutaja mahali watakoweka kambi kwa kuogopa kufanyiwa ushirikina.Karne hii na mtu mwenyewe msomi bado anaaamini upuuzi.Ndio maana tunafungwa na watani wetu kwani imani kama hizo zinawatia wachezaji hofu na kuwaathiri kisaikolojia.Wachezaji wanaletewa waganga wa kienyeji eti watasaidia timu kushinda.Tuache hizo mpira ni sayansi.Na bado kuna watu wanatetea ujinga huu ili kuganga njaa.

Anonymous said...

NI AIBU KUBWA TIMU KAMA YANGA KUWA NA KIONGOZI WA OVYO KAMA MADEGA. YEYE KAMA MWENYEKITI NA KAMATI YAKE NZIMA HAWANA LOLOTE WANALOFANYA ZAIDI YA KUTEKELEZA ASEMACHO MANJI. NI AIBU KUBWA.

KWA HALI INAVYOENDELEA WNAYANGA TUJIANDAE. VIONGOZI HAWA NI WEZI KUPINDUKIA. MWENYEKITI NA MSAIDIZI WA MANJI WAMEUNGANA KULA PESA NA KUWAACHA VIONGOZI WENGINE WADUWAA. ZANZIBAR VIJANA HAWAKUCHEZA KWA MOYO KWA SABABU MADEGA ALIPEWA MILION 4, LAKINI YEYE AKAWAPA LAKI NANE TU NA WALA KAMBINI HAKUFIKA. BILA KUJALI KUWA WAMEKAA SOUTH AFRICA KWA TAABU BILA POSHO WALA NINI.

LET US BE CAREFUL.

Anonymous said...

Mechi leo imekwendaje??Yanga vs Miembeni