Friday, February 01, 2008

Kibaruani leo na Wagosi

Ligi Kuu ya Vodacom inaendelea tena leo kwa vijana wetu wa Jangwani kujitupa katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam kupepetana na Coastal Union ya Tanga.

Mchezo huo unatarajiwa kuwa wa kulipiza kisasi kwani katika mchezo wa kwanza, Yanga ililala 1-0 huko kwenye Uwanja wa Mkwakwani Tanga.

Hadi sasa Yanga inashikilia nafasi ya pili katika msimamo wa ligi kwa kujikusanyia pointi 24 ikiwa ni pointi 3 nyuma ya vinara wa ligi hiyo Prisons ya Mbeya.

Kila la heri Yanga.

3 comments:

Anonymous said...

vipi huko mbona kimia

Anonymous said...

Keeeep Up Yanga!

Anonymous said...

Jamani vipi matokeo ya mpira?