Friday, February 29, 2008

Tupeni raha JangwaniRaha tulizopata mwaka jana dhidi ya Petro Athletico

Wapinzani wa Yanga katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, AS Adema ya Madagascar inatarajiwa kuwasili nchini leo kwa ajili ya pambano la marudiano la raundi ya awali litakalopigwa katika Uwanja wa Taifa keshokutwa.

Wakati timu hiyo ikiwasili leo, Yanga ipo katika maandalizi makali kujiandaa na pambano hilo na imekuwa ikiwakataza mashabiki kuingia uwanjani kuangalia mazoezi hayo.

Katika mchezo huo ambao utaamuliwa na waamuzi kutoka Sudan, Yanga inatakiwa kushinda si chini ya 2-0 kufuatia kipigo cha 1-0 wiki mbili zilizopita huko Madagascar.

Viingilio katika mchezo huo vimepangwa kuwa 20,000/= (VIP), 15,000/= (Main Stand), 8,000/= (Green Stand) na 3,000/= (Mzunguko).

Mpira unadunda, lakini kama siku hiyo ukitudundia vizuri basi ushindi wa 2-0 unawezekana. Mzee mzima Sunguti, akina Chuji pale kwenye kiungo na kwenye ulinzi kuna Cannavaro - bila shaka watatutoa vifua mbele hiyo Jumapili.

Panapo majaliwa mimi nitakuwa Uwanjani kuwadondoshea yale yatakayojiri huko kupitia hapo chini kwenye comments.

YANGA DAIMA MBELE.

22 comments:

Anonymous said...

all the best lakini tell that guy sunguti akaze legelege sana wazee, he knows everything but is not forcing goals, man nakosola nayebite.....

Anonymous said...

mwaikimba vipi mkubwa mbona hivyo, unatuangusha bwana wewe kaza tu buti uwazibe watu midomo kitaeleweka tu simba wanachonga sana bro.
Nicodemus Minde, NAIROBI UNIVERSITY

Anonymous said...

Asante mzee, nitakuwa nachungulia hapa ili kupata latest. Yanga waisiegemee sana 2-0, kwani inawezekana wageni wakaanza kupata goli au wakasawazisha 1-1 au 2-2, la muhimu Yanga ni kutumia vizuri nafasi zote watakazopata na kulinda goli kwa pamoja. Hata ikiwa 5-3 sio mbaya. Kisaikolojia inaweza kuwaathiri kama wamejiwekea 2-0 halafu wageni wakaanza kufunga.
M.E., Berks, UK

Anonymous said...

nawatakia kila la kheri vijana watang'ara salamu toka kuwait kwa wana yanga wote

Anonymous said...

Kila la heri wana Yanga wote.

Nitakuwa online pia kufuatilia matokeo jinsi itakuwa inaendelea.

Mdau,
Zack

Anonymous said...

mimi natabiri goli 5 ,mtaona .mr mwanza.

Anonymous said...

Niko USA nasubiri kwa hamu please naomba yoyote yule atume habari haraka kuhusu mchezo. asanteni wanayanga wote.

Anonymous said...

tuko nyuma yenu vijana wa jangwa ushindi utakao watoa adema ndio furah kwetu zingatieni mafunzo ya condic tunamuamini sana .Paul kabewa Serbia

Anonymous said...

Huyu Mwaikimba, toka kuja kwa Condic amekanyaga uwanjani muda kidogo saana.
Hivi alikuwa akipangwa na Chamngwana kwa jina tu bila kujali kiwango chake?
Sasa hivi naona jina halichezi nafikiri ni mwanzo mzuri maana hata Mwalala anasugua benchi ile mbaya.
Mlioko bongo mnasemaje?

Anonymous said...

Mpira utaanza saa 10 kamili. Kikosi ni Haule, Mbuna, Maftah, Ndhlovu, Nadir, Yusuf, Ngassa, Chuji, Sunguti, Abuu na Credo

Anonymous said...

Tunaanza 2nd half. Bado ni 0-0

Anonymous said...

Tunaongoza 1-0 kupitia kwa Sunguti

Anonymous said...

2-0 Sunguti tena

Anonymous said...

Mpira umekwisha, tumeshinda 2-0

Anonymous said...

Vipi mliokuwa uwanjani, hebu tupeni hali ya mchezo ilikuwaje? maana ingawa tumeshinda lakini wasiwasi wangu hawa Madagascar kiwango chao ni cha chini saana. Ingawa magoli si muhimu kuwa mengi cha muhimu timmu kama inacheza kitimu na mashambulizi ya kupanga.

Anonymous said...

NAWASHUKURU YANGA KWA KUZINGATIA MAAGIZO YA MWALIMU USHINDI NDIO FURAHA YETU

Anonymous said...

Ahsanteni kwa ushindi sasa tunamtaka mnyama yanga imara daima nahangaika kupata habari kwenye magazeti bado hamna mpya nipo kuwait najiunga na wana yanga wote ktk hii sherehe ya ushindi ila tuzingatie ligi hatutaki kupoteza point tena yanga yanga yanga

Anonymous said...

huree kazi nzuri sana wamefanya vijana kweli wanastahiri pongezi na asanteni sana kwa wale waliokuwa wanalete matokeo mtandaoni mungu awabariki sana YANGA MBELE DAIMA
LUSEKELO SANTIAGO DE CUBA

Anonymous said...

Kiwango bado sana.Timu bado inahitaji marekebisho ya hali ya juu.Bado tunacheza bora liende.Kwa mpira huu hatufiki mbali.Mchezo wa jana nilivyouona haunipi matumaini yeyote.

Anonymous said...

Huyo anonymous wa mwisho hapo juu (1:51:00 PM) bila shaka ndio yule wa msimbazi aliyetuleleta matokeo ya Yanga vs Mtibwa hapa. Siammini kwamba in a well contested match ambapo tulihitaji magoli 2 kusonga mbele, kwamba tumeyapata kwa kubahatisha tuu. Lazima tukubali kuna kazi imefanyika. Marekebisho kweli yanatakiwa (hata Arsenal wanayafanya kila mara) lakini si kwa kiwango anachosema huyo 'mdau'!

Anonymous said...

Wewe ano wa 5:46 wacha ujinga wa kufuata mkumbo.Mimi ni Yanga damu na sio wafuata mkumbo.Sikusema tumepata magoli kwa kubahatisha.Nimesema timu inahitaji marekebisho na bado haichezi kama timu.Kufunga magoli sio tija sana kwani unaweza kufunga ukacheza vibaya na unaweza kufungwa ukacheza vizuri.Suala ni kuwa na constructive critisism ili kujenga timu yetu.Kuwapa label wanaokosoa hakusaidii.Kwenye mada inayofuata mwenye blog amesema marekebisho yanahitajika na yeye ni Simba.Tuache ujinga na tuwe wakweli tuache kufuta mkumbo kikondoo.

Anonymous said...

"....
Akizungumzia mchezo huo, kocha wa AS Adema, Franck Rajaomarisamba aliusifu mchezo na kuwasifu Yanga zaidi kuwa ni timu kali na itafika mbali. Hata hivyo aliwapongeza vijana wake kuwa walicheza kwa nguvu lakini bahati haikuwa yao.

..."

Source: http://mwananchi.co.tz/newsre.asp?id=4801