Wednesday, February 27, 2008

Yanga kupaa zaidi leo?
RAUNDI ya pili ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, inaendelea tena leo kwa mechi moja baina ya vinara Yanga dhidi ya Mtibwa Sugar, mechi itakayochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Yanga iliyo na pointi 36 na kufuatiwa na Prisons kwa pointi 35, inashuka dimbani kwa shingo upande baada ya kukwama kwa ombi lake la kutaka kusogezwa mbele kwa mechi hiyo.

Yanga ilitaka kuahirishwa kwa mechi hiyo ili iweze kujiandaa vema kwa mechi yake ya kimataifa dhidi ya AS Adema ya Madagascar, itakayopigwa Jumapili.

Mechi hiyo dhidi ya AS Adema, ni ya marudiano baada ya ile iliyopigwa wiki mbili zilizopita iliyoisha kwa Yanga kufungwa 1-0, hivyo Yanga kulazimika kushinda 2-0 katika mechi ya Jumapili.

Ushindi katika mechi ya leo pia itakuwa ni muhimu katika kujenga morali ya wachezaji kabla ya pambano lake hilo muhimu dhidi ya AS Adema.


9 comments:

Anonymous said...

Tutakuwa tunasubiri matokeo. Asante.

Anonymous said...

Mechi si imeshaanza?

Zach

Anonymous said...

mpira upo katika lala salama na hadi sasa ni 1-1

Anonymous said...

Mpira umekwisha kwa kipigo cha 2-1.

Tumeshindwa kujikita kileleni mwa ligi Kuu ya Vodacom. Tugange ya Jumapili dhidi ya AS Adema

Anonymous said...

Oops...

Vp tena?

Anonymous said...

Mbona magazeti yanasema ni 1-1? Au goli moja limefutwa baada ya mechi kuisha?

Anonymous said...

Kuna mdau asiyeitutakia mema ametaka kuwarusha roho kwa kutoa matokeo ya Yanga kufungwa.

Kumbe hata mashabiki wa Simba huwa wanapita kwenye blog hii? Kwanini wasianzishe ya kwao?

Yanga Daima mbele, nyuma mwiko.

Anonymous said...

hata mimi nilivunjika moyo baada ya kusoma tumelala ,lakini baada ya kusoma magazeti, roho ilipumua loo? afadhali tumepata pointi.

Anonymous said...

Huyu bwege aliyesema kuwa tumelala alinikosesha amani ya kufanya kazi leo kutwa nzima, kwa sababu matokeo huwa nayapata asubuhi kabla ya kwenda kazini.
Kumbe tofauti!! dah!!! mungu amlaani najua atakua simba tu huyu, any way yote maisha ndivyo watu tulivyo,wacha maisha yaendelee, na YANGA daima mbele nyuma awepo huyu mkichaa aliyenikosesha amani kwa saa kadhaa yeye na simba yake.
Shenzi kabisa huyu.
Mwana YANGA HALISI.
Japan.