Thursday, March 06, 2008

Kondic atishia kujiuzulu
Kocha Mkuu wa Yanga,Dusan Kondic ametishia kujiuzulu timu hiyo iwapo mfumo wa uendeshaji wa soka hapa nchini hautabadilika.

Kondic, ametoa kauli hiyo kutokana na ubovu wa ratiba ya Ligi Kuu ya soka ya Tanzania Bara, ambapo amesema kuwa haitoi nafasi kwa kocha kufundisha kikamilifu timu yake.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kondic alisema kuwa hayuko tayari kufundisha katika mazingira magumu ya Ligi Kuu, ambayo yamelenga kudidimiza soka.

Alisema kuwa ratiba ya Ligi Kuu imebana sana, ambapo timu inalazimika kucheza mechi kila baada ya siku tatu, kitu ambacho hakitoa mapumziko kwa wachezaji.

Kondic, alitolea mfano kwa timu yake, ambapo alisema kuwa katika mwezi uliopita alipata nafasi ya kufundisha mara nne huku timu yake ikicheza mechi saba.

Alisema, mfumo huo hautoi nafasi kwa Kocha kutoa maelekezo kikamilifu, ambapo inafikia wakati wachezaji wanacheza bila kufuata mfumo.

Aidha, aliongeza kuwa ni vema wapangaji wa ratiba wakaliangalia suala hilo upya ili kutoa nafasi kwa makocha kutekeleza majukumu yao, ambapo alitaka angalau timu icheze mechi moja kwa wiki.

Kocha huyo alisema kuwa hajui ni kwa nini Ligi imepangwa kumalizika mapema wakati kulikuwa na uwezekano wa ligi hiyo kumalizika mwezi Mei bila kuathiri tarehe za FIFA.

Yanga hivi karibuni ilicheza na mechi mbili za Kombe la Shirikisho dhidi ya AS Adema Madagascar pia katika kipindi hicho ilicheza mechi kadhaa za Ligi Kuu zilizokuwa zimepangwa karibu karibu.

NIPASHE

7 comments:

Anonymous said...

Wadau: Nani mwenye ukweli hapa: Kondik ama TFF?

--------------

Shirikisho la soka lashuku uwezo wa kocha wa Yanga toka Serbia
Na Phillip Nkini

SHIRIKISHO la Soka Tanzania TFF limesema lina wasiwasi na uwezo wa kocha mkuu wa timu ya Yanga, Dusan Kondic, kutokana na kauli zake kwenye vyombo vya habari.


Kondic juzi alizungumza na vyombo vya habari na kusema kuwa atajiuzulu endapo Shirikisho la soka halitakubali matakwa yake ya kurekebisha ratiba ya Ligi kuu inayosdababisha timu icheze mechi moja kila baada ya siku tatu pamoja na kuita wachezaji wachache kutoka kwenye klabu na kwenda timu ya Taifa.


Akizungumza na Mwananchi jijini jana Mkurugenzi wa Soka wa Shirikisho hilo Sunday Kayuni amesema anawasiwasi na uwezo wa kocha huyu kutokana na kauli zake alizozitoa kwa kuwa kama kocha mwenye uelewa asingetakiwa kuzungumza hivi.


"Kondic namheshimu lakini anakasoro kama angekuwa ni kwa kuwa yeye ni kocha alitakiwa afike kwanza kwenye sekretarieti azungumze nayo sio kukurupuka na kuzungumza tu,


"Nina wasiwasi na uwezo wake wa kufundisha, kwani awali tuliwapa muda mrefu sana na wadau wakasema Ligi imesimama muda mrefu sana lakini ule muda tuliwapa ili wajiandae, na wengine waliwapeleka wachezaji wao Afrika Kusini na wengine Mwanza"alisema Kayuni.



Akizungumza kuhusu suala la miundombinu, Kayuni alisema Shirikisho la soka limekuwa likishunghulikia kwa nguvu zote kuhakikisha kuwa Ligi inapata mdhahmini lakini sio kazi yake kujua timu inakwenda kucheza Ligi mkoani kwa kutumia usafiri gani kama ni ndege au gari.


Alisema ratiba ya Ligi inapopangwa viongozi wa timu zote zinazoshiriki ligi hushirikishwa kuhusu hilo na huo wanaalikwa wanaowanatoa maoni yao.


Naye Katibu mkuu wa Shirikisho hilo Fredrick Mwakalebela alisema hiki sio kipindi cha kufanya mazoezi kama kocha huyu anayotaka bali alitakiwa kufanya mazoezi kabla Ligi haijaanza.


Alisema Kocha wa Yanga hakuzingatia ufundi bali alilizungumzia suala hili kisiasa zaidi, kama wakiangalia Simba wametoka Ethiopia wakaelezea nini watafanya dhidi ya Enyimba hayo ndio maandalizi.


Alisema kama kocha huyo anaona kuwa timu yake imebanwa na ratiba basi wanatakiwa wacheze chini ya kiwango ili wasiwe mabingwa ili wacheze Ligi ya ndani tu.


"Timu za Ulaya zinacheza mechi tisini Klabu bingwa Carling FA Klabu Bingwa na michezo mingine lakini makocha wao hawalalamiki bali wanapanga mikakati ya ushindi kwa mwaka kwetu nchini ambapo wachezaji wanacheza mechi arobaini tu ambazo ni sawa na nusu ya Ulaya"alisema.


Katibu mkuu wa Chama cha makocha Tanzania Eugen Mwasamaki alisema akizungmzia hili alisema kwa kipindi cha Ligi huwa hakuna suala la muda wa mazoezi bali ni muda wa kufanya masahihisho ya mechi uliyocheza jana.


Aliendelea kusema suala la kuwa na wachezaji wengi timu ya Taifa ni sifa kubwa kwa klabu lakini anashangaa kuona kocha huyu anakasirika pale wachezaji wake wanapoitwa kwenye timu hiyo.


''Nashagaa kuona eti kocha anachukua wachezaji wake kuitwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa, siku zote hatua ya kwanza ya soka ni klabu na baada ya klabu ni timu ya sasa ni kitu cha kushangaza kuona kocha anakataa wachezaji wake kuwa kwenye hatua ya juu zaidi hatua aliyokuwa anatakiwa kujisifu nayo" alisema.


Alisema kama kanuni zinafauatwa hakuna kitu chochote kibaya kwa hili bali kama timu ipo kwenye Ligi ndio inatakiwa kusimamishiwa michezo yake ikitoa zaidi ya wachezaji watano.


Source: www.mwananchi.co.tz

Anonymous said...

MAONI YANGU NI HAYA ,AFADHALI HAO MAKOCHA WAENDE KULIKO YANGA NA WANACHAMA WAKE WAONWE KAMA HATUNA AKILI NA WATANI ZETU.PILI NAOMBA VIONGOZI WETU WAACHE TABIA YA KUCHUNGULIA DIRISHANI KUONA SIMBA WANAFANYAJE,HII NI KUHUSU RUFAA YAO KWANINI TUNAWAPA SUPPORT COASTAL ,WENYEWE WATAJIJUA WANA KATIBA YAO KAMA SIMBA,TFF,YANGA ,NAOMBA TUJALI YETU.KWAHERI .MWANZA

Anonymous said...

Hata mimi nilishawahi kumsema/kumlaumu huyu kocha jinsi anavyotumia vyombo vya habari.

Nilimlaumu sana aliposema kuwa wachezaji wa Yanga wakapime kwanza kabla ya kuripoti kambini.
Tena aliwahi kusema eti wachezaji ni wagumu kuelewa mafundisho kwa vile hawajui kiingereza! Hana habari Carlos Tevez, Nani, Anderson wa Manchester United, Fernando Torres wa Liverpool, Reyes aliyekuwa Arsenal wote hawaelewi kiingereza lakini kazi zao uwanjani kila mtu anazifahamu.
Huyo Kondic anaongea vitu asivyoelewa, ndio maana hata Sunady Kayuni anamshuku uwezo wake!
Nadhani maoni yangu sasa yanaanza kupata uzito/'sapoti'.

Inawezekana sana uwezo (na ujuzi??) wake kama kocha wa timu ni mdogo! (ingawa sina ushahidi lakini kivitendo anajionyesha mwenyewe)!!!

Lakini Yanga nao wana sera ipi kuhusu Vyombo vya habari (PR)?

Anonymous said...

Kondic ni kocha mzuri, anachosemma kina ukweli kabisa chukulia msimu uliopita wachezaji wa yanga walikuwa na mashindano mengi na wengine walikwenda Brazil na timu ya Taifa wakaa muda mrefu. Matokeo yake ilikuwa ni kazi ya ziada kwa Micho kuwaunganisha kwenye programu na wengine. Kingine walikuwa wamechoka mno kwa kucheza muda mrefu bila mapumziko ndo maana hata tukapoteza ubingwa.
Timu ya taifa haiwezi kuwa ikila mara inakwenda mazoezi ya mwezi, wapi na wapi? Huyu Maximo msanii hamna kitu, soon mtajionea. Kuhusu Kayuni, hebu niambie ni timu gani amewahi kufundisha ikapata mafanikio???
Ni kheri angeongea mtu kama Minziro au Kibadeni, Msomali lakini si huyu.

Anonymous said...

Mimi nianze na hii habari (http://mwananchi.co.tz/newsre.asp?id=4906) kocha wa prisons akilalamika ratiba kuwa inawachosha wachezaji wake hadi kasi yao imepungua sana, sasa sijui naye uwezo wake ni mdogo au TFF wanasemaje?

Naaminini alichosema Kondik ni sawa kitaalamu na sina wasiwasi na uwezo wake, badala yake nina wasi wasi mkubwa na uwezo wa Kayuni na Maximo kwa sababu zifuatazo:

1. Makocha wengi (akiwemo Kayuni na Maximo) wamekuwa wakisema timu ya taifa haifanyi vizuri sababu wachezaji hawajaandaliwa kwenye timu zao. Wakati huo huo, wanasema wakati wa ligi sio wa kuandaa wachezaji, sasa wanataka kusema wachezaji wanafundhidwa kwa mwezi mmoja tuu kabla ligi haijaanza, na mafunzo hayo ndio yanatosha mwaka mzima! This is a joke and big contradiction!

2. Wanasema hata timu za Uingereza (England) zinacheza mechi nyingi (90) kuliko za Tanzania. Wanasahau kuwa wenzetu ratiba ya mwaka mzima ikiwa pamoja na mechi za kimataifa inatoka kabla mwaka haujaanza, na hakuna timu inayocheza mechi kila baada ya siku 2 kwa mwezi mzima bila kupumzika (huku ikisafiri kati ya Bukoba, Dar na Mbeya kwa basi). Ratiba ya Barclays league ina breaks nyingi kwa timu zote. Ratiba ya TFF haijaandaliwa kiufundi (kitaalam), hilo ndio alilowaambia Kondik, nao badala ya kutafakari kwanza wakakurupuka kumjibu bila facts. Mfano: Yanga baada ya kutoka Madagasca, ilitakiwa kucheza mechi 4 kati ya Dar, Mwanza, Kagera, etc kabla ya mchezo wa marudiano. Hii ni kama vile TFF hawakujua Yanga itacheza michezo ya CAF wakati wanapanga ratiba, ndo maana wanaahirisha michezo ya ligi ili Yanga/Simba zicheze michezo ya kimataifa.

3. Alicholalamikia Kondik juu ya timu moja kuwa na wachezaji wengi timu ya taifa sio tuu idadi wa wachezaji, bali huu utaratibu wa Maximo na TFF kuita wachezaji hadi 7 toka timu moja wa wakakaa na timu ya taifa kwa mwezi mzima au zaidi. Utaratibu wa FIFA ni siku 5, kwa nini TFF hawakujibu hili. Wachezaji wanatakiwa kufunsishwa mpira kwenye timu zao, na Maximo akiwaita anahitaji siku 5 tuu kuwaunganisha wacheze kama timu (kama kweli ni kocha mwenye uwezo anaotaka tuamini kuwa anao), hatakiwi kuwafundisha mpira, sio kazi yake. Hiyo ni kazi ya kina Kondik, ndio maana wanataka wawe na muda wa kufanya hiyo.

4. Kocha yeyoye mzuri anatakiwa aweze kwa mfano kurekebisha/kubadilisha mfumo wa uchezaji wa timu yake wakati ligi inaendelea. Atawezaje kufanya hivyo kama kila baada ya siku 3 ana mechi mara tanga, next Mbeya, then Dodoma, na usafiri ni wa barabara?

5. TFF wenyewe walichelewesha kuanza kwa ligi kisa walikuwa bize na timu ya Taifa, wakasahau kuongea na mdhamini wa ligi. (This is being irresponsible!) Wamejuka kukurupuka muda umeisha wanapanga ratiba bila vigezo vyovyote vya kitaalamu, na wakiambiwa wanakuwa wakali kama mbogo, ebo!

Yako mengi tuu, lakini muhimu nadhani ni kwa TFF kukubali kupokea maoni hata yake ambayo hawayapendi, maana bado tuko nyuma, sasa tusipokubali kujifunza kama tff walivyo hatutafika popote.

Zack,

Anonymous said...

Zack,
Soma hii hapa
Carlo Ancelotti admits it wasn’t a vintage Milan performance. “We’re still on the road to recovery.”

The 3-1 victory away to Empoli put them within a point of fourth place, but they needed two goals in the last five minutes to achieve the result.

“Aside from the points, I didn’t like Milan today,” confessed the Coach. “We are still on the road to recovery.

“We can’t seem to play with fluidity, but thankfully this was the last game in a packed fixture list and from tomorrow we will be able to train normally.”

Ancelotti has blamed their poor form and Champions League exit on the fact the Club World Cup revolutionised their calendar, forcing the team to play twice a week since January 13.

“We struggled to get these three points, but it was very important to win today. It was also a fortunate round considering Fiorentina lost at Siena, but there’s a long way to go yet.

“It is not something I’ve had to say in recent years, but we don’t have to play Cup games and that can be an advantage.”

Roma are the only Italian side still in the competition, awaiting Inter’s second leg against Liverpool on Tuesday.

“Now it is inevitable we’ll all be cheering on Roma. They have more experience to do better than before. I am an ex-Giallorossi player, so it’s no problem for me to admit I hope they win more than Inter.”

Ancelotti has been put under the microscope following the defeat to Arsenal and it’s reported next year’s revolution will include a new Coach.

“We are building the future together. I am in sync with the club and we agree on everything, including the fact that a total revolution is unnecessary. Let’s not lie – a few players will change, but that’s it.”

Alberto Malesani is under pressure amid rumours defeat today would see him sacked and replaced by his predecessor Gigi Cagni.

“I would make all the same choices again,” assured the Empoli boss. “Milan only changed the game in the final minutes when our players were struggling with cramp.”

Anonymous said...

Zack,

Ulyoandika hamna cha kuongezea, hapa ndo utajua ni kwa nini soka la bongo halitakuja kukua.