Monday, March 03, 2008

Mwendo wa Kiarabu sasa!
Al Akhdar ya Libya

Baada ya kuiondosha AS Adema ya Madagascar hapo jana kwa jumla ya 2-1 (2-0 , 0-1) Yanga sasa itakumbana na timu za Afrika ya Kaskazini ikianzia na Al Akhdar ya Libya.

Al Akdar imebahatika kuingia hatua inayofuata bila jasho baada ya wapinzani wao Tourbillon ya Chad kuzuiwa na CAF kushiriki michuano hiyo, baada ya chama cha soka cha nchi hiyo kuwa na madeni ndani ya Shirikisho hilo.

Katika mchezo huo utakaofanyika kati ya Machi 21, 22 na 23, Yanga itaanzia ugenini na wiki mbili baada ya hapo itaialika Al Akhdar Jijini Dar.

Endapo Yanga itavuka hatua hiyo, bado itaendelea kupambana na Waarabu wengine kwani ratiba inaonyesha kwamba mshindi anatakiwa akutane na mshindi kati ya Mouloudia (Algeria) na Haras El Hodoud (Misri).

Tuanze sasa kufanya maandalizi kwani kwa kiwango cha jana, timu yetu inaonekana bado inahitaji maandalizi makubwa sana. Bila shaka mwaka huu ule woga uliokuwa umejengeka kwa Yanga kwamba hawawezi kuzitoa timu za kutoka nchi za Kiarabu utatoweka.

Inshallah.

5 comments:

Anonymous said...

UWEZO WAKUWATOA WAARABU TUNAO KINACHOTAKIWA NI MAANDALIZI YA UHAKIKA ALL THE BEST YANGA

Anonymous said...

UWEZO WAKUWATOA WAARABU TUNAO KINACHOTAKIWA NI MAANDALIZI YA UHAKIKA ALL THE BEST YANGA

Anonymous said...

Libya tunawatoa hamna wasi.
Timu (Yanga) ijiandae na TFF isaidie timu kwa kupanga vizuri ratiba ya ligi ili Yanga ipate nafasi ya kujiandaa. Sijawahi kuona chama cha soka kinaigandamiza timu yake ktk ratiba za ligi ya ndani -isipokuwa TFF!!!!

Anonymous said...

mpira wa libya si wa kutisha kujipanga vizuri mechi za majaribio zanguvu natumai raudi ya pili tumepita tff haiangalii maendeleo ya soka bali kipato kiasi gani kimepatikana mlangoni msijali wana yanga umoja ni nguvu vita mbele sakran q8

CM said...

kumradhi wadau mwanzoni nilisema tutaanzia nyumbani lakini baada ya kuangalia vizuri ratiba, nimeona kwamba tutaanzia ugenini na baada ya wiki 2 tutakuwa wenyeji hapa Dar.

Asanteni.