Tuesday, April 29, 2008

Ivo, Nsajigwa warejeshwa Stars

KOCHA Marcio Maximo amewarudisha wachezaji Ivo Mapunda na Shadrack Nsajigwa kwenye kikosi cha timu ya taifa kilichoanza kambi jana kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa raundi ya pili ya michuano mipya ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) dhidi ya Uganda.

Ivo Mapunda na Shadrack Nsajigwa walifungiwa kwa miezi sita na uongozi wa klabu ya Yanga kwa madai ya utovu wa nidhamu na adhabu yao iliisha Aprili 26.

Adhabu hiyo iliwalazimisha waondolewe kwenye kikosi cha Stars baada ya kuidhinishwa na Shirikisho la Soka (TFF).

Kurejeshwa kwa wachezaji hao, kunafanya Yanga kuwa na jumla ya wachezaji 9 katika kikosi hicho. Wachezaji wengine ambao wapo Stars ni Fred Mbuna, Amir Maftah, Nadir Haroub "Cannavaro", Abdi Kassim, Mrisho Ngassa, Jerry Tegete na Athumani Iddi "Chuji".

3 comments:

Anonymous said...

kocha maximo hafai kwasababu anachagua wachezaji ambao hawafundishiki.kocha bora ni kama yule anayeenda kuchagua yosso ambao wanafundishika,hatutafika mbali.

World of Soccer said...

Si kweli kwa hicho unachokisema, Maximo ni Kocha wa timu ya Taifa si kocha wa timu ya Vijana. Maximo ni victim wa mfumo wetu wa soka,mfumo wetu hauvumbui vipaji vipya.

Kawaida kocha wa timu ya taifa kazi yake ni kuassemble best players katika nchi na kuwapa strategy ya mchezo.

Kwa timu za wenzetu hata hapo Senegal wachezaji wanafanaya match analysis ya michezo ya wapinzani ili waweze kuona udhaifu upo wapi ili wao wawabane vipi.

Lakini hata hivyo maximo amejitahidi sana kutumia vijana wadogo. Wengi walimtukana sana alipowaita kina Jerry Tegete, Maregesi Mwangwa,Vicent Barnabas etc. Lakini vijana hao sasa hivi ni wachezaji wa kutumainiwa na timu zao.

Anonymous said...

can some body tell me if yanga is going to promote under 20 or from team b .ile ya chamangwana ? au ilikua geresha ya kuunda timu ili wawagereshe tff?kama ipo hiyo wachezaji gani wanapandishwa timu a.asante