Sunday, April 20, 2008

Yanga Bingwa 2007/08

Yanga imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, baada ya kutoka sare ya 2-2 na Prisons ya Mbeya katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa Dar.

Kwa sare hiyo, Yanga sasa imefikisha pointi 48 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yeyote katika ligi hiyo ambayo inashirikisha timu 14.

Hata hivyo licha ya Yanga kujitangazia ubingwa mapema, kuna tishio kutoka kwa wapinzani wetu wa jadi Simba ambao wanakusudia kukata rufaa katika Baraza la Dunia la Rufaa za michezo CAS kudai kurudishiwa pointi zao tatu ilizonyang'anywa baada ya kumchezesha mchezaji aliyekuwa amefungiwa. Endapo Simba itashinda rufaa hiyo na ikifanikiwa kushinda mechi zake mbili zilizosalia, itakuwa imejikusanyia pointi 49.

Pamoja na ndoto hizo za alinacha za wenzetu ambao viongozi wao wanahaha kutafuta pa kutokea mbele ya wanachama wao, sisi ni wakati wetu wa kucheza mechi zetu mbili zilizobaki bila shinikizo.

Tunawapongeza wachezaji kwa kazi kubwa waliofanya.

7 comments:

Anonymous said...

naomba usajili ufanywe kwa umakini sana kwani tunahitaji aina ya wachezaji wenye moyo na nia njema ya kuchezea klabu yetu

Anonymous said...

mie nakuunga mkono vijana wadogo wakikaa pamoja naamini timu itabadilika badala ya kutumia majina makubwa fedha nyingi mchezo duni au tunauguza msimu wooote m sakran

Anonymous said...

VIONGOZI WETU WA YANGA (MABINGWA 2008) TUNAWAOMBA MUWE MAKINI NA MECHI KATI YETU NA KAGERA SUGAR TUWEKE MIKAKATI YA KUHAKIKISHA TUNASHINDA TENA KWA MABAO MENGI TU ILI WATANI WETU WA JADI WAKATE TAMAA NA HIYO RUFAA YAO WANAYOTAKA KUKATA. KWANI TUKIWAFUNGA KAGERA SUGAR TUTAFIKISHA POINTI 51 AMBAZO HATA HAWA WATANI WETU WAKIRUDISHIWA HIZO POINTI WANAZOZITAKA IKIWA PAMOJA NA KUSHINDA MECHI ZOTE ZILIZOSALIA HAWATAWEZA KUFIKISHA POINTI HIZO 51 !!!!!!!!!! UNAJUA PAMOJA NA KUWA WANATISHIA MTU MZIMA NYAU LAKINI WANAWEZA KUKATA KWELI RUFAA NA IKAKUBALIWA !!!! HIVYO TUWEMAKINI NA HIYO MECHI NA KAGERA SUGAR !!! VIONGOZI CHONDE CHONDE CHONDE !!!!

Anonymous said...

Hongera vijana

Anonymous said...

nichokoze tu, hivi hii aibu ya majengo chakavu na timu kuwa bila uwanja ili hali ule wa kaunda upo itaisha lini?????

je viongozi wetu wana mtizamo wa kimaendeleo?????.

nipongeze juhudi za kumsajili yosso wa Ngorongoro heroes Zaid Ismail ni kinda mzuri sana atatusaidia ni mrefu ana umbo la kimpira. anamapenzi ya dhati na Yanga.

amaekulia Mwanza akiwa na akina Tegete,Ngasa na Henry Joseph akafichuliwa na kipingu yuko Makongo secondary.

ni kiraka anacheza namba 2, 7, 9 na 4

Anonymous said...

Ni aibu klabu kubwa kama Yanga eti haina uwanja wa mazoezi, inakwenda kugombea uwanja wa Taifa!

Naamini kama tungekuwa na viongozi kama wa sasa (simaanishi kina Madega tuu bali wote tulionao for the past 2 decades) hata Yanga yenyewe isingekuwepo. Tuangalie maendeleo yaliyokuwepo enzi zile za Mzee Tabu Mangara na wenzake, na leo!

Sasa hivi hata kupaka majengo rangi ni shughuli ambayo haiwezekani.

Tunahitaji viongozi wenye uwezo wa kuunganisha wapenzi na wanachama na kuleta maedeleo ktk karne hii!

Anonymous said...

HONGERA KWA MCHANGO WAKO MZURI, NAONA HAWA JAMAA WAMEKALIA KUTAFUNA VIJISENTI TOKA JENGO LA VIOO NDIYO MAANA ETI WANAPAITA BUZWAGI!!!!!!!!!!!!!
NINA PRESHA NA MECHI YA LEO SIJUI NITAJIFICHA WAPI TUKIFUNGWA