Friday, May 09, 2008

Kondic amtaka Yondani Jangwani

Kelvin Yondani

Kocha Mkuu wa klabu ya Yanga Dusan Kondic huenda akakabiliwa na wakati mgumu katika kuwapata wachezaji wapya anaowataka, baada ya kuweka bayana kwamba anamtaka Kelvin Yondani wa Simba pamoja na Stephen Mwasika wa Tanzania Prisons ya Mbeya. Huo umekuwa ni mtihani kutokana na viongozi wa klabu ya Simba kuweka wazi kuwa hawako tayari kumuachia mchezaji huyo, ambapo walisema wameshaingia nae mkataba kwa ajili ya kuitumikia timu hiyo msimu ujao.


Hali pia huwa si nzuri kwa wachezaji wanaohama kutoka Prisons ya Mbeya kwani katika miaka ya nyuma wachezaji kama Henry Morris, Samson Mwamanda na Primus Kasonso waliletewa misukosuko mikubwa baada ya kuachana na timu hiyo inayomilikiwa na Jeshi la Magereza.


Mwenyekiti wa Klabu hiyo Imani Madega, hivi karibuni alikaririwa na baadhi ya vyombo vya habari akisema kuwa Yanga kwa sasa inaouwezo wa kumsajili mchezaji yeyote bila kujali gharama. Hata hivyo, aliyekuwa kocha wa timu hiyo Mserbia Micho aliwaasa Yanga kusajili wachezaji wenye viwango, lakini sio wale wanaotoka nchi jirani ya Kenya kwa kuwa ni wasumbufu wakubwa.

5 comments:

Anonymous said...

jee tutawapandisha wale wachezaji wa chamangwana ?mimi nataka kujua ,tafadhali hebu nipeni mwanga kidogo.

Anonymous said...

Sina hakika kama umefika wakati wa kuwapandisha vijana wa Chamangwana. Lakini katika kuwafuatilia kwenye mechi wanazocheza pale Taifa kabla ya mechi za Yanga, nimeona kuna watatu wanazo sifa za kupandishwa; Kipa, Sentahafu (mrefu sana, mweupe, anasoma Makongo Secondari) pamoja na kiungo wa mbele. Lakini Prof. Kondik atawapima kwani huwa anakuwepo kuwa-assess.

Kwa upande wa Yondani, namkubali sana. Ni mchezaji mzuri na aliyetulia mno. Ananikumbusha Hayati Methord Mogella alivyokuwa anacheza, akipangwa kama libero. Kuna sifa nyingine ambayo inamuongezea Yondani sifa za kujiunga na Yanga; ni mapenzi makubwa aliyo nayo kwa wana Jangwani. Yondani, Henry Joseph, Ngassa, Tegete na Amir Maftah, wamefundishwa mpira pamoja na Bwana John Tegete (Baba yake Jerry Tegete) pale Mwanza. John Tegete kwa sasa ni Manager wa CCM Kirumba. Kwa mujibu wa Tegete, vijana hao wote ni Yanga Damu. Yeye mwenyewe Tegete ni mshabiki mkubwa sana wa Yanga, na mwaka huu ameweza kum-scout beki mzuri sana wa kushoto toka Toto Africa ambaye atatua Jangwani baada ya kupimwa na Kondik. Kwa wanaomfahamu huyo kijana wa Toto, he could be the best left back in the Country!

Anonymous said...

Tukiweka ushabiki pembeni: Hivi kuna mkataba usioweza kuvunjwa? Nadhani ifike mahali tuache mambo ya ujima; kama timu inamtaka mchezaji kichotakiwa kugomba ni dau tuu, sio 'hatuwezi kumruhusu aende Yanga au Simba'.

Leo Wenger akimtaka Christiano Ronaldo,anachofanya ni kutangaza dau, kama Man-U bado wanamtaka wanaongeza, otherwise wanamuachia. Hivi ndivyo namna value ya mchezaji inavyoongezeka.

Analogy ama mfano mwingine: Microsoft wametoa offer ya kuinunua Yahoo. Sio kwamba Yahoo walishasema wanataka kuuza kampuni yao. Ni kwamba mtu yeyote akitoa offer, unatakiwa uikubali, au uikatae kwa kutoa sababu za msingi (kibiashara); na issue kwamba hii ni kampuni yangu sii sababu ya msingi!

Nakubaliana na Mrisho Ngassa kutaka apewe mkataba mpya. Ngassa aliyesaliwa wakati wa Micho miaka 2 iliyopita sio huyu wa sasa. Amepata uzoefu mkubwa zaidi na kupandisha kiwango chake. Kama Yanga bado inamtaka, inamwongezea mkataba mwingine wenye masilahi zaidi. Same case for Henry Joseph, kama Simba bado wanamhitaji wampe mkataba mzuri kuliko offer atakayopewa na Yanga, halafu aamue mwenyewe anataka kukaa/kwenda wapi!

Anonymous said...

asanteni wote kwa habari hizi.mimi naenda nyumbani mwanza ,kupumzika alafu ntarudi hapa usa. nataka nipate habari zote mwenyewe ,mimi yanga hasa si unajua tena asanteni.

poker said...

PROMO DELIMA
poker online terpercaya | poker online | Agen Domino | Agen Poker | Kumpulan Poker | bandar poker | Judi Poker | Judi online terpercaya | bandar qiu | situs judi online

Ayo segera daftarkan diri anda dan bergabunglah bersama kami !!
Delimapoker.com Situs Agen Poker Online Terpercaya di Indonesia akan melayani Anda dengan profesional, memproses depo/wd dgn cepat. Come join and be a winer with us !!

Untuk info selanjutnya silakan chat ke :
Livechat_____: delimapoker
BBM__________: 7B960959
Facebook_____: delimapoker
Phone number_: +85595678845
pendaftaran___