Monday, July 28, 2008

CECAFA yailima Yanga
Baraza la soka la Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) limetoa adhabu kwa klabu ya Yanga kufuatia kitendo chake cha kugomea kuleta timu uwanjani kupambana na Simba katika mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu wa Kombe la Kagame iliyokuwa ipigwe hapo jana kwenye Uwanja mkuu wa Taifa.

CECAFA imeipiga Yanga kifungo cha miaka 3 ya kutoshiriki michuano hiyo endapo itafanikiwa kutwaa ubingwa wa Tanzania Bara na mbali ya kifungo hicho pia klabu hiyo imetakiwa kulipa faini ya dola za Kimarekani 35,000 ambazo zinatakiwa kulipwa ndani ya miaka 3.

Aidha CECAFA imeitaka Shirikisho la Soka nchini TFF kuiadhibu klabu hiyo kwa ngazi ya kitaifa. Tayari TFF imesema itatoa tamko hapo kesho.

10 comments:

Anonymous said...

vingozi wafungiwe maisha.wametuaibisha sana.

Anonymous said...

Mbona walipoihangaisha Yanga kuwapa pesa hamkusema shirikisho livunjwe? Hili shirikisho ni la ubabaishaji mtupu

Anonymous said...

Uongozi Yanga unatia kichefuchefu. Adhabu ndogo iongezwe. Waende kwa Manji kuomba kulipiwa.

Anonymous said...

Eti hawakupewa milioni 100 kwa timu 2! Huu ujinga. Zawadi zenyewe zote 3 hazizidi milioni 65, iweje simba na yanga wapewe milioni 100 tena katika nafasi ya tatu bila kujali wameshinda au kushindwa! Madega sema ukweli uliogopa kipigo. Sababu yako ni ya kitoto. Sasa unaibebesha yanga adhabu ya dola 35,000 na kifungo. Huna maana uongozini yanga. ONDOKA.

Anonymous said...

Yanga walikosea kutopeleka timu uwanjani (hata kikosi B tu kingetosha!)

Pia nadhani hata mfadhili wao alichangia kuwaambia viongozi wasipeleke timu uwanjani; nao wakamtii.

UPEO wa viongozi wetu wa soka ni mdogo/mfinyu sana! Hata yule msemaji wa CECAFA naye ana upeo mdogo kwa kuzingatia lugha na maneno aliyotumia ktk kutangaza adhabu dhidi ya Yanga.

Anonymous said...

Waungwana mmeiona adhabu ya TFF kwa Yanga? Yaani sasa Yanga ni sawa na timu ya mchangani kwa miaka 2. Wachezaji walio stars ndio watapata bahati kucheza mechi za kimataifa. Hata hivyo, nao wanaweza kutemwa maana hawatakuwa na mechi ngumu za kupima uwezo wao ili wateuliwe na Maximo. Isitoshe, morale ya mpira itawaishia. Usajili wa milioni 400 umeishia kuua vipaji vya wachezaji na timu yote. Kina Madega wameua Yanga. Na mabilioni ya Manji hatuyataki tena! Yameua Yanga!

Anonymous said...

Ni vema kufa maskini kuliko kujazwa mapesa ukakosa kauli. Ona sasa Yanga, Manji katujaza manoti kayeyusha akili za viongozi. Kila kitu "YES". Msipeleke timu uwanjani "YES bwana mkubwa",mpeni Kaseja milioni 35, "YES tajiri", nitawapeleka Uingereza "YES mzungu wetu". Haya sasa, miaka 2 hakuna kucheza hata na shule ya msingi ya Kenya!!! Kuna timu hapo!!!

Anonymous said...

sasa kwa kuwakomoa yanga itachukua ubingwa wa bara mara tatu mfululizo, bila mazoezi wala nini. adhabu ya cecafa itatekelezwa ndani ya mipaka ya cecafa.
ngoma ipo kwa tff. sasa wamewafungia yanga kucheza mechi za kimataifa wakati wameiacha icheze ligi ya nyumbani!! hapo nao wamenikanganya kwa sababu kama yanga atachukua ubingwa mara mbili basi tz bara itawakilishwa na timu zisizo bingwa ktk mashindano ya kimataifa.
kuhusu wachezaji kuchezea timu ya taifa, maximo anachukua wachezaji toka mashindano ya ligi, na siyo mechi za kirafiki... kwa hiyo wachezaji wa yanga bado wanayo nafasi ya kuchezea timu ya taifa kama viwango vyao vitaruhusu.

BAADA YA KUSEMA HAYO: ni kweli yanga walikosea kutopeleka timu na wanastahili adhabu. lakini adhabu zenyewe zilivotolewa hazionekani kuwa zina lengo la kuendeleza soka. ktk ligi za wenzetu mtu akifanya makosa anatozwa faini, na ikiwa kosa ni kubwa sana basi anapunguziwa pointi kwenye msimu ujao wa ligi: kwa mfano leeds united ya uingereza walipokoknywa pointi kabla hata msimu haujaanza, hayo pia yamejitokeza kwa timu ya luton juzijuzi tu.
lakini unaposema 'marufuku kucheza mechi za kirafiki? hapo hata cecafa na tff wamebofoa!

Anonymous said...

Ndugu Yangu najua una nia nzuri katika kutoa mawazo.YANGA wamefanya kosa kwenye CECAFA hivyo TFF wamefuata ushauri wa CECAFA wa kuiadhibu Yanga kwenye michezo ya kimataifa.Na kwa sababu CECAFA ipo affiliated na CAF basi timu yetu itakosa mechi za CAF.Kuhusu mifano ulitoa Yanga haiwezi kuwa deducted points kwa sababu haikugomea mchezo wa ligi ya ndani.Utawa deduct point kwa kanuni gani???Adhabu tuliyopewa ni kwa makosa manane.Pia Madega na Lucas wamepewa siku 7 wapeleke ushahidi wa makubaliano ya kupewa milino 50 kabla ya mechi kabla ya TFF kuwachukulia hatua.Viongozi wetu wametuweka kwenye wakati mgumu wa kujinasua kwenye tatzizo hili.Kuna jamaa yangu mabye yupo karibu sana na uongozi ameniambia kwamba tatizo halikuwa pesa bali kipa kwa sababu Kaseja alipata udhuru na Ivo alikataa kucheza akisema kwamba anaogopa lawama kwani mechi ya Moro alilaumiwa bila sababu za msingi.Hivyo hatukua na kipa.

Anonymous said...

wote mmeongea vyema, lakini adhabu ya CECAFA aiwezi kuiua YANGA kwa kuwa Regulation zake ni tofauti na CAF, huwezi kuharibu CECAFA ukafungiwa CAF, kwa nini, eleza sababu za msingi sio kwakuwa kuna mtu wa YANGA kasema, tatizo letu tunaona mtu akiwa jikoni ndio kashiba sio kweli
Robert.B